Laptop hii itakufaa kwa matumizi ya Nyumbani, Ofisini na Safarini

Mwandishi Diana Benedict

Kampuni ya kichina inayojihusisha kutengeneza smartphones, TV, Earphone na Powerbank zinazojulikana sana Xiaomi, Mwaka 2016  kwa mara ya kwanza ilizindua Laptop yake ya kwanza Xiaomi Mi NoteBook. Xiaomi inakuja kwa aina mbili tofauti, kwa ukubwa wa 13.3-inch na 12.5-inch. Laptop za kwanza kufanana na MacBook Air, ambazo zinakuja katika ukubwa wa 13.3-inch na 11.6-inch.

Mi Notebook ni nyembamba kuliko Macbook, wakati Apple ya 13.3 inch ikiwa na wembamba wa 17mm na uzito wa 1.35kg, Inch 13.3 ya MiBook ina wembamba wa 14.8mm na uzito wa 1.28kg.

Na Macbook Air ya 12.5 inch ina wembamba wa 17mm na uzito wa 1.08kg, MiBook yenyewe ina wembamba wa 12.9mm na uzito wa 1.09kg tu.

ff4cf14e32c2dfa86eb58848cf420921 1
Xiami Notebook 13.3” na Macbook 13.3”

Hapa nimefananishishia na Laptop za Apple Macbook kwakuwa laptop za Macbook ni very popular, Laptop ya Xiaomi Notebook ni rahisi kubebeka na ni nyepesi kushinda ya Macbook, Mfano katika laptop ya 12.5 inch ina uzito wa 1.09kg tu na body ya Aluminium kwa laptop nzima!UntitledXiaomi Notebook: Design & Specification

Xiaomi Notebook Zimetengenezwa kwa Aluminium Body na zinakuja kwa Aina mbili tofauti, ile ya Inch 13.3 na ile ya Inch 12.5, Processor ya Intel Core M3 na Intel Core i5, Zote zikiwa na Onboard RAM ya 4gb, na 8gb tu, Pia Kwa storage Xiaomi imeinclude Onboard SSD kuanzia 128GB, 256GB na 512GB Inategemea na chaguzi utakalofanya wakati wa kununua.

Xiaomi Notebook ina Graphic User Interface GPU ya Nvidia GeForce 940MX inayokutosheleza kabiosa kwa ajili ya kazi zako ya Kudesign mfano Adobe Photoshop, Kuplay Games zenye Graphic kubwa kama FIFA 2017.

Xiaomi Mi Notebook inakuja na Pre-Installed Microsoft Windows 10, Operating System ambayo ni Popular kwa  Siko la computer duniani inayotumia na computer nyingi dunia zilizobase kwa IBM kama HP, Lenovo, Dell na Acer na unaweza ku update mpaka Windows 10s yenye ulinzi Zaidi.

xiaomi mi notebook air the description of all models in the mi laptop series 001

Xiaomi Notebook: Battery & Colours

Ninatumia Simu ya Xiaomi Mi5 zaidi ya miezi mitano sasa, naweza sema kampuni ya Xaomi ni kampuni inayojitahidi kutengeneza battery zeney ubora katika vifaa vyao, Na sasa ni wiki na nusu Natumia Laptop hii ya Xiaomi 13.3 Inch yenye 40Wh Batterry natumia Zaidi ya masaaa 12 bila kuchomeka charg.

Iko hivi naweza kuondoka asubuhi kwenda kazini nikaacha charg yangu ya laptop nyumbani nikaenda kazini na kufanya kazi zangu nikarudi jioni na bado laptop ina charg ya kuendelea na kazi nyingine.

Laptop hizi zinakuja na Rangi mbili tofauti katika hii ya 13.3 ni Gold na Spacegray au Silver, (Mini natumia ya Silver) na vivyo hivyo kwa laptop ya inch 12.5

Xiaomi Notebook: Bei na Upatikanaji

Kwa sasa sina uhakika wa duka hapa Tanzania linalouza Laptop za Xiaomi lakini unaweza agiza Ebay au Aliexpress kwa Bei ya 600USD bei rahisi kabisa ukilinganisha na tumiaji ya Macbook.

Tufuatilie @MtaawaSaba ili usipitwe na Habari, Uchambuzi naMakala mbali mbali ya mitanadoni na ya kiteknolojia kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Google+ na Youtube, Pia usisite kutoa maoni yako hapo chini au tuandikie barua pepe kwa mhariri@mtaawasaba.com

Mwandishi Diana Benedict Mwandishi
Mitandao ya Kijamii
Diana Benedict. Digital Creator | IT Specialist | Graphics Designer | Web Designer | Web SEO | Contents Management | UI/UX Designer and Social Media Management.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive