Mambo 6 ya kufanya, na Simu janja yako itakuwa salama

Mwandishi Alexander Nkwabi
Simu ya mkononi kama ilivyo kompyuta zingine, ina mapungufu yake. Mara kadhaa ushasikia kuhusu app zinazoweza kuharibu simu yako au ishu za usalama wa simu yako kwa ujumla. Makala hii itakuangazia mambo Mambo 6 ya kufanya

Kuna mtazamo ambao watu wanaona kama vifaa vinavotumia mfumo endeshi wa Apple yani iOS ni salama zaidi kuliko watumiaji wa Android. Huwezi amini miezi kadhaa iliyopita kulikuwa na shambulio lenye jina la Spectre lililolenga simu za mkononi na halikuchagua cha Android wala iOS wote walikuwa hatarini, hata hivyo mwezi tisa mwaka jana kampuni ya usalama ya Sophos Labs iligundua zaidi ya 30% ya shambulio la Ransomware lilikumba watumiaji wa Android ambapo yapata App zipatazo milioni 10 na zaidi ziliwekewa alama kama zenye kutia mashaka na mienendo yake.

Mpaka hapo tunaona hakuna simu iliyo salama moja kwa moja, basi soma Mambo 6 ya kufanya, na Simu janja yako itakuwa salama na kupunguza uwezekano wa kuiweka simu yako kwenye hatari.

Lock simu yako

Hakikisha una lock simu yako, hii ndio hatua ya awali kabisa katika kuiweka simu yako salama. Kwa kufanya hivyo unawazuia watu wengine kuweza kuchezea simu yako ikiwemo kunistall app ambazo hujawaruhusu kufanya hivyo pia unawazuia wale wanaopenda kusoma soma meseji wakishika simu ya mtu.

Simu za siku hizi ulinzi wa lock umerahisishwa sana kuliko mwanzo ambapo ulilazimika kuingiza tarakimu kadhaa au kuchora pattern, sasa hivi kuna njia zingine mbadala, salama na rahisi kutumia baadhi ni finger print lock na face recognition na hata iris scanner ambapo simu itajifungua baada ya kumulika macho ya mwenye simu.

Hakikisha una set muda mfupi wa simu kuji lock yenyewe ili hata kama itaangukia mikono isiyo salama iji lock haraka

Hakikisha mfumo endeshi wa simu yako haupitwi na wakati

Utafiti unaonesha watumiaji wengi wa simu uwa hawa update mifumo endeshi ya simu zao. Hii ni hatari na kuiweka simu katika hatari. Hakikisha una sasisha matoleo mapya kadiri yanavyotoka. Kama simu yako haiwezi kupokea masasisho mapya huo ndio wakati wa kununua simu mpya. Na kama unataka kununua simu mpya chunguza kwanza itaendelea kupata masasisho mapya kwa muda gani kabla haijapitwa na wakati.

Taarifa kutoka Fossbytes mwa 2018 zinaonesha ni asilimia 1.1 tu ya watumiaji wanatumia toleo la Android Oreo na asilimia 28.5 pekee ndio wanatumia Android Nougat na watumiaji sawa na asilimia 12 wanatumia Android Kitkat

Kwa watumiaji wa Apple wao wana nafuu maana taarifa inaonesha asilimia 70 wanatumia iOS 11.2 na watumiaji sawa na asilimia 10.1 wanatumia matoleo ya nyuma kuanzia 10.3 kurudi nyuma

Chagua Simu zenye majina yanayojulikana

Makampuni yanayojulikana kwa kawaida uwa wanatoa masasisho kwenye simu wanazotoa kuliko kampuni ambazo hazijulikani sana. Lakini hii isikuzuie kununua simu ya bajeti nafuu, hata hivyo kuwa makini kabla hujafanya manunuzi, jiridhishe kwanza.

Kadri simu inavozidi kuwa ya bei nafuu ndio inavokuwa inatia mashaka katika kupata updates kwenye simu iyo japo kuna simu za bei nafuu na zinapata updates.

Fanya Encryption

unapoifanyia encryption simu yako unaweka taarifa za simu yako salama, ikitokea simu yako ikaangukia mikononi mwa watu wabaya hawataweza kugusa taarifa zako. Mchakato wa encryption ni rahisi ila kama huelewi, tutakuchambulia zaidi kwenye makala ingine.

Weka Antivirus

Siku za mwanzo wa matumizi ya simu janja kuweka antivirus haikuwa lazima sana, lakini kutoka na kupamba moto kwa matumizi makubwa ya vifaa vinavyobebeka, imefanya watu wabaya na wahalifu kuhamishia nguvu zao kwenye simu za mkononi na vifaa vingine vinavyobebeka.

Nenda kwenye duka la app na pakua antivirus yako mara moja na uanze ku scan virus na mipangilio mingine ambayo inaweka simu yako kwenye risk.

Kwepa kui jailbreak au ku root simu yako

Watumiaji wengi wa iPhone na Android wanapenda ku jailbreak au ku root simu zao ili kuwezesha simu zao kufanya mambo mengi zaidi na kwa ufanisi zaidi. Pamoja na kuwa na faida pia kuna hasara zake, mfano kama utadownload app nje ya app store zinazojulikana zinaweza kuleta shida kwenye simu yako maana zina uwezo wa ku access system files bila ruhusa yako.

Mfano mwaka 2015, KeyRaider ilikuwa ni malware iliyolenga simu za iPhone zilizokuwa jailbroken, matokeo yake akaunti za Apple zipatazo 225,000 zikadukuliwa. Kwa upande wa android malware inayoitwa CopyCat ilifanikiwa kuathiri simu takribani milioni 14. Na vyanzo zilikuwa ni izi app za kujidownlodia tu wenyewe kwenye site zisizoeleweka.

Kwa Sababu za kiusalama ni heri usi root au ku jailbreak simu yako.

Haya ndiyo Mambo 6 ya kufanya, na Simu janja yako itakuwa salama. Endelea kutembelea tovuti yetu na usisahau kutufuata kwenye mitandao ya kijamii.

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive