Kampuni ya huduma za kifedha ya NALA yakusanya bilioni 23.1 za uwekezaji

Mwandishi Emmanuel Tadayo
Kampuni ya kitanzania inayotoa huduma za kifedha ya NALA yakusanya bilioni 23.1 za uwekezaji.

Fedha hiyo ambayo ni sawa na dola za kimarekani milioni 10 imekusanywa kutoka kwa wawekezaji wakiwemo Amplo, Accel, na washirika wa Bessemer, pia kwa ushirikiano na wachangiaji wengine wakiwemo waanzilishi wa kampuni za Monzo, Robinhood, Alloy na Deel. Pia NALA inatarajiwa kuanzisha kampeni ya uchangiwaji mwaka huu na watumiaji wa mwanzo wataweza kumiliki hisa kwenye kampuni ya NALA.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, kampuni ya NALA imepanua wigo wa utoaji huduma za kutuma na kupokea fedha ambapo mwanzoni ilikuwa ni ndani ya nchi tu, sasa itawezesha kutuma na kupokea fedha kutoka Uingereza kwenda nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Ghana. Kwa mujibu wa NALA, takribani watumiaji 8000 wamefanya miamala yenye thamani zaidi ya dola za kimarekani millioni 10 kwenda nchi kadhaa za Afrika ndani ya miezi sita iliyopita.

Afrika ni moja ya maeneo ambayo ni ghali sana kutuma na kupokea fedha, kwa gharama za wastani wa asilimia 10.6, watoa huduma zakifedha za kidijitali kama NALA wanatamba kwa wateja wao kama watoa huduma wenye viwango vya chini kabisa vya kutuma na kupokea fedha, wameripoti TechCrunch.

Kufuatia makusanyo haya, NALA inatarajia kutanua huduma zake na kufikia nchi 12 za kiafrika ikiwemo Nigeria mpaka kufikia mwisho wa mwaka huu, pia inatarajia kuzindua huduma za kuhamisha fedha Marekani na nchi za ulaya ndani ya robo ya kwanza.

Akiongea na gazeti la The Citizen, Mkurugenzi mtendaji bwana Benjamin Fernandes alisema NALA itatumia fedha hizi kuboresha miundombinu ili kurahisisha huduma zao, ” Naamini huduma za malipo kwenye bara la afrika zimetengenezwa kwa asilimia 1, tunahitaji teknolojia sahihi kuhakikisha miundombinu inasimikwa ili kuwezesha mifumo ya huduma za kifedha barani afrika”.

Kwa sasa takribani asilimia 80 ya fedha zinazotumwa Afrika hutumwa kwa njia ya fedha taslimu, na asilimia 20 iliyobaki ndio pekee huamishwa kwa kupitia mikondo ya kidijitali ambayo hata hivyo hukumbwa na changamoto nyingi ikiwemo gharama kubwa za makato kwenye huduma hizo.

Mwandishi Emmanuel Tadayo Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
mwandishi wa habari za teknolojia kwenye tovuti pendwa ya mtaawasaba
1 Comment

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive