Nokia 8110 yarudi ikiwa na 4G, Facebook na kifuniko cha Matrix

Mwandishi Alexander Nkwabi

Pamoja na simu zingine 4, kampuni iliyo nyuma ya utengenezaji wa simu za Nokia ya HMD Global imezindua simu ya Nokia 8110 (ambayo ilipewa jina la utani “banana phone” kutokana umbo lake) kwenye maonesho ya Mobile World Congress jijini Barcelona na kuleta msisimko wa miaka ya 90 wa kile ki slider. Kama wewe ni mpenzi wa sinema na filamu lazima utakuwa unaikumbuka simu hii iliyojizolea umaarufu kupitia kwenye filamu ya The Matrix iliyoigizwa na Keanu Reeves.

nokia8110bananayellow3 png 256895 original

Kutokana na mauzo mazuri ya simu ambayo pia ilirudishwa upya ikiwa imeboreshwa ya Nokia 3310, HMD wakaona walete simu ingine ya zamani ikiwa imeboreshwa kurudisha msisimko wa miaka hiyo.

Muonekano na Kioo

RqtbPvTYXTH2CAYh7NWZAA 650 80

Simu hii imetengenezwa kwa plastiki, na kwa sababu iyo tunategemea simu hii itakuwa ngumu zile simu za Nokia za enzi izo. Cha kusisimua zaidi ni kava linalofunika keypad ambalo lina slide hivyo kurahisisha zoezi la kupokea na kukata simu.

Kioo Cha simu kina ukubwa wa inchi 2.4 na kina QVGA (160 x 120) na pia sio touch sensitive. Vitufe vyote kwenye simu hii viko kwenye keypad kama ilivyo kwenye simu zingine ambazo ni za kawaida. Kioo kinatosha kabisa kwa kuandika ujumbe mfupi, kucheza game, na vitu vingine vidogovidogo

Nokia 8110 4G ina patikana kwa rangi mbili nyeusi na ya njano yenye msisimko wa hali ya juu ‘banana yellow’. Pia ina sehemu ya kuchomeka headphone, bila kusahau redio ya FM

Mfumo endeshi na uwezo wake

nokia8110bananayellow7 png 256899 original

Simu hii inakuja prosesa ya Qualcomm 205 na  RAM 512MB pekee, ambazo zinatosha kabisa kuruhusu mfumo endeshi wa Smart Feature OS unaopewa nguvu na Kai OS.

HMD wamesema simu hii ambayo inakuja na intaneti ya kasi ya 4G mpaka sasa app zilizothibitishwa kufanya kazi na simu hii ni pamoja na Facebook, Twitter, Google Maps na Google Assistant. na unaweza kuigeuza WiFi hotspot na ukasambaza intaneti kwa vifaa vingine.

Pamoja na hayo, Moja ya mambo mazuri kabisa kuhusu simu hii ni kuja na game la Snake lililoboreshwa kabisa  ambalo tulianza kuliona kwenye 3310 mwaka jana.

Kuna kamera yenye 2MP upande wa nyuma na flash ya LED ambayo haikuwepo kwenye simu ya mwanzo, hakuna kamera ya mbele kwenye simu hii

nokia8110bananayellow5 png 256897 original

Mwisho simu hii ina betri inayotoka yenye 1500mAh ambayo ina uwezo wa kukuruhusu kuongea na simu mpaka masaa 9.32 ukiwa kwenye VoLTE, na siku 25 ikiwa haitumiki.

Bei ya Nokia 8110 4G

Simu hii ya kawaida itaingia sokoni ikiuzwa kwa dola za kimarekani karibu 100 sawa na laki mbili na 20 za kitanzania. Bei hii ni kubwa ukilinganisha na 3310 mpya kwa sababu kadhaa ikiwemo gharama kubwa zilizotumika kutengeneza simu iliyojikunja, pia ina teknolojia ya 4G ambayo imeongeza wigo wa matumizi ya simu hii ndogo.

Simu hii itaanza kuwa madukani kuanzia mwezi wa tano mwaka huu ambapo tarehe haijawekwa wazi.

Endelea kuwa nasi kwa kutufuata kwenye mitandao ya kijamii, na usisahau ku subscribe ili uwe wa kwanza kupata Habari, Uchambuzi na Makala mbali mbali za kisayansi na teknolojia. Pia usisahau ku acha maoni yako hapo chini na unaweza kuwasiliana nasi kwa barua pepe mhariri@mtaawasaba.com

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive