MtaawasabaMtaawasaba
  • Habari
  • Simu
  • Android
  • Kompyuta
  • Windows
  • Maujanja
  • StartUps
Mengineyo
  • Muongozo
  • Maujanja
  • Programu
  • Simu Janja
  • Teknolojia
Mtaawasaba
  • Kuhusu Sisi
  • Sera ya faragha
  • Vigezo na Masharti
  • Wasiliana Nasi
Mitandao
  • Facebook
  • Twitter
  • Instagram
  • YouTube
  • Newletters
© 2013 - 2023 Mtaawasaba Interactive
Unasoma Qualcomm yagomea ofa ya kununuliwa na Broadcom kwa Dola Bilioni 121
MtaawasabaMtaawasaba
  • Apple
  • kompyuta
  • Maujanja
  • Apps
  • StartUps
  • Magari
  • Mtaawasaba
    • Habari
    • Makala
    • Apps
    • Maujanja
    • Kompyuta
    • Simu Janja
    • Magari
    • Matukio
    • Muongozo wa mtumiaji
    • Mitandao ya kijamii
    • Programu
    • Teknolojia
    • Mfumo endeshi
    • Miwani Janja
    • Saa Janja
    • Televisheni
    • Utamaduni
  • Mengineyo
    • Microsoft
    • intaneti
    • Windows
    • SnapChat
    • TTCL
    • Tigo Tanzania
    • vifurushi visivyo rasmi
    • Google
    • halotel
    • Instagram
    • iOS
  • Kuhusu Mtaawasaba
    • Kuhusu Sisi
    • Sera ya faragha
    • Vigezo na Masharti
    • Wasiliana Nasi
Una akaunti? Ingia
Tufuate mtandaoni
© 2022 Mtaawasaba Interactive. Haki zote zimehifadhiwa.
Mtaawasaba > Featured > Qualcomm yagomea ofa ya kununuliwa na Broadcom kwa Dola Bilioni 121

Qualcomm yagomea ofa ya kununuliwa na Broadcom kwa Dola Bilioni 121

Imeandikwa na Alexander Nkwabi Miaka 5 iliyopita
Sambaza
Qualcomm yagomea ofa ya kununuliwa na Broadcom kwa Dola Bilioni 121

Bodi ya wakurugenzi wa kampuni inayotengeneza semiconductor ya Qualcomm kwa pamoja wagomea dili ya dola za kimarekani billioni 121 kununuliwa na kampuni ingine inayotengeneza semi conductor ya Broadcom

Katika maelezo yao mbele ya waandishi wa habari, bodi ya wakurugenzi wa Qualicomm ilisema kuwa kiasi cha dola 82 kwa shea kilikuwa hakitoshi na kiliishushia thamani ( japo kama ingekubalika basi ingekuwa ni dili kubwa kuliko yote kuwahi kutokea ulimwengu wa elektroniki.)

Unaweza Kusoma

Elon Musk ametangaza rasmi vita na Apple

Ramani, kutoka Tanzania yakusanya $32m kurahisisha mnyororo wa usambazaji

Teknolojia ya hali ya juu kutumika katika Kombe la Dunia la FIFA Qatar 2022

Tovuti ya iCloud ya Apple yapata muonekano mpya, inavutia zaidi.

Broadcom walisema ofa hii ni kubwa na ya mwisho, baada ya kuongeza asilimia 15 ya ofa yao ya mwanzo iliyotangazwa mapema mwezi ya kumi na moja 2017 ambayo ilikataliwa, ilikuwa ni ya dola za kimarekani  billioni 105. Akizungumza na gazeti la New York Times, Mkurugenzi mtendaji wa Broadcom, bwana Hock Tan alisema ofa kama hii ilitakuwa kukubaliwa na bodi yoyote.

Broadcom ambayo kwa sasa makao makuu yake ni Singapore ina mpango wa kuhamishia makao makuu yake nchini Marekani baada ya bwana Tan kuonana na raisi wa Marekani Donald Trump kwenye ikulu ya White House.

Kama Qualcomm ingekubali kununuliwa na Broadcom ingeifanya kampuni hiyo kuwa kampuni kubwa ya tatu duniani kwa utengenezaji wa semiconductor nyuma ya Intel na Samsung electronics. Muungano wa kampuni izo mbili ungewezesha utengenezwaji wa vifaa ambavyo ningetumika kutengeneza simu janja zaidi ya bilioni moja kila mwaka.

Ofa hii imekuja wakati kipindi kigumu kwa Qualcomm ambayo imekumbwa na mgogoro mkubwa kisheria na kampuni ya Apple ambapo Qualcomm imeadhibiwa na Umoja wa Ulaya faini ya dola za kimarekani billioni 1.2 baada kugundulika kuwa walikuwa na lengo la kuwazuia wapinzani wao kama intel kufanya kazi. Qualcomm wamesema watakata rufaa kuhusiana na faini hiyo.

Hisa za Qualcomm hivi karibuni zimekuwa zikishuka thamani baada ya ripoti kuwa Apple inataka kuachana nao na kufanya kazi na kampuni pinzani ya intel badala yake.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Mtaawasaba, pia usisahau ku subscribe kama bado hujafanya hivyo  ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka kila zinapotoka tu.

 

 

KWENYE Apple, Broadcom, Intel, Qualcomm
Sambaza chapisho hili
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Telegram Barua Pepe Nakili kiungo Durufu
Acha Ujumbe

Toa Jibu Ghairi kujibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Mtaawasaba Newsletter

Jiunge nasi kwa njia ya barua pepe tukujulishe kila inapotoka habari mpya

Zaidi Kutoka Mtaawasaba

Sasa unaweza pata Blue Tick kwa kulipia Instagram na Facebook

Sasa unaweza pata Blue Tick kwa kulipia Instagram na Facebook

Siku 4 zilizopita
Airtel yawa ya kwanza kuzindua huduma ya kadi za eSIM Tanzania

Airtel yawa ya kwanza kuzindua huduma ya kadi za eSIM Tanzania

Siku 5 zilizopita
Instagram yazindua Notes, Candid Stories, na Zaidi

Instagram yazindua Notes, Candid Stories, na Zaidi

Miezi 3 iliyopita
Umoja wa Ulaya waishinikiza Apple kuruhusu maduka mbadala ya programu kwenye iPhones na iPads

Umoja wa Ulaya waishinikiza Apple kuruhusu maduka mbadala ya programu kwenye iPhones na iPads

Miezi 3 iliyopita

© 2013 - 2023 Mtaawasaba Interactive. Crafted by Simba Creative

  • Kuhusu Sisi
  • Sera ya faragha
  • Vigezo na Masharti
  • Wasiliana Nasi
Go to mobile version
logo logo
Karibu Mtaawasaba!

Jaza taarifa kuingia Kwenye Akaunti Yako

Umesahau Nywila?