Samsung Galaxy S9: kuzinduliwa Februari 25

Mwandishi Alexander Nkwabi

Ni muda sasa kumekuwa na tetesi za simu mpya kutoka kwa kampuni mashuhuri ya kutengeneza vifaa vya ki elektroniki ya Samsung. simu hizo ni Samsung Galaxy S9 na Samsung Galaxy S9+.

Katika tangazo la kuwakaribisha watu wa habari katika uzinduzi wa simu hizo ambalo wao huliita “Unpacked” limetoka likionesha tarehe ya uzinduzi kuwa ni mwezi wa pili tarehe 25 ikiwa ni siku moja kabla ya kuanza kongamano kubwa la wadau wa mawasiliano ya vifaa mkononi (mobile) linalojulikana kama Mobile World Congress ambalo litafanyika huko Barcelona Hispania kuanzia tarehe 26 mwezi wa pili mpaka tarehe 1 mwezi wa tatu.

samsung galaxy s9 mwc invite
Tangazo la mualiko kutoka Samsung

Taarifa zilizovuja kuhusu simu za Samsung Galaxy S9 na S9+ zinaonesha mabadiliko kadhaa yanayokuja na simu hizi mbili ikiwemo sehemu iliyopo finger print sensor itakuwa chini ya kamera tofauti na watangulizi wake S8, S8+ na Note8 kuwa na fingerprint sensa pembeni ya kamera na kufanya iwe ngumu kwa watumiaji kuifikia.

Pia inasemekana kutakuwa na maboresho makubwa kwenye kamera ambapo S9+ inasemekana itakuwa na kamera mbili kwa nyuma. Taarifa zilizovuja zinaonesha S9 itakuwa nakioo chenye ukubwa wa inchi 5.8 QuadHD+ AMOLED, kamera ya nyuma yenye megapikseli 12 na ya mbele yenye megapkseli 8. Pia RAM 4GB na uwezo wa kuzuia vumbi na maji.

DUedA6zWkAAYerd
Muonekano wa Samsung Galxy S9 na S9+ kama ilivooneshwa na mvujishaji maarufu Evan Blass

Simu zote mbili zinatarajiwa kuwa na sehemu ya kuchomeka head phone, hata ivyo utaweza kutumia headphone zenye waya na ambazo hazina.

Endelea kutembelea Mtaawasaba.com kwa taarifa zaidi za kiteknolojia ambazo tunaendelea kukupa kila zinapojitokeza

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive