Samsung yazindua Diski ya SSD yenye ukubwa wa Terabyte 30

Mwandishi Alexander Nkwabi

Yapata miaka miwili sasa tangu Samsung waachie diski yenye ujazo wa Terabyte 15.36 ambayo kwa wakati huo ilikuwa kubwa kuliko zote kupata kutokea duniani.

Leo wamezindua (Solid State Drive) diski ambayo imepewa jina la PM1643, ina ujazo wa Terabyte 30.72, mara mbili ya ujazo wa diski iliyokuwa ikishikilia rekodi, na hivyo kuivunja rekodi hiyo na kuwa SSD kubwa kuliko zote duniani. Madhumuni ya kutengeneza diski hii ni kwa ajili ya kutumika kwenye mifumo ya kuhifadhi taarifa za taasisi za kiserikali, mashuleni na mahospitalini.

Diski hii ya PM1643 iko kwenye kisanduku chenye ukubwa wa inchi 2.5 pekee, ndogo eeeh? Toleo hili lina uwezo kuandika data wakati kunakili kwa kasi ya 2,100MBps na 1,700MBps wakati wa kusoma data, ambayo ni kasi mara tatu zaidi ya hard diski za 860 Evo na Pro ambazo pia hutengenezwa na Samsung.

Utengenezaji wa SSD hii ya PM1643 umeanza tangu mwezi wa kwanza mwaka huu na wanatarajia kuendelea kutengeneza pia SSD zenye ujazo mdogo kuanzia 15.36TB, 7.68TB, 3.84TB, 1.92TB, 960GB na 800GB.

Hata hivyo haijajulikana ni lini SSD hii itaingia sokoni, wala bei yake haijajulikana kwa sasa. Wala usitegemee kuona SSD hii kwenye laptop na kompyuta zingine siku za hivi karibuni.

Je, Unajua tofauti kati Solid State Drive na Hard Disk drive? Tunadikie  hapo chini na maoni yako. Pia usisahau kutufuata kwenye mitandao ya kijamii na ku subscribe ili uendelee kupata habari motonoto za teknolojia kila zinapotoka.

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive