Kampuni ya TECNO ni kampuni ya Kichina inayojohusisha na uzalishaji wa bidhaa za kielectroniki hususani simu za mkononi. Kampuni ya Tecno ilianzishwa mnamo mwaka 2006 chini ya Tecno Telecom Limited lengo lake kuu ikiwa ni kuzalisha Simu za bei nafuu zaidi ikilenga soko la Afrika. Na hii ndiyo Siri ya TECNO kuongoza zaidi ya Asilimia 50% kuuza bidhaa nyingi Tanzania.
TECNO ilianza kuzalisha simu ya Smartphone ya kwanza mwaka 2012 TECNO P3 ambayo ndio ilikuwa smartphone ya kwanza kuuzwa bei nafuu zaidi Tanzania kwa mwaka huo ikifuatiwa na Models kama Tecno N3, M3, P5 kwa mwaka 2013.
Kwanini inaendelea kufanya vizuri katika Soko la Afrika hususani Tanzania?
1: Kuzalisha smartphone za Bei ya chini
Ninapochagua kununua Smartphone kuna mambo ya kuangazia lakini kabla ya hapo naangalia bajeti ya mfuko wangu. Kampuni ya Tecno ndiyo kampuni inayozalisha smarphone za bei ya chini Afrika hususani Tanzania. Tecno inazalisha simu zinazotumia Chipset Za Mediatek ambazo zinajulikana kuwa ni chipset za gharama nafuu katika utengenezaji.
2: Betri inayotunza umeme kwa muda mrefu
Katika kutunza umeme simu za Tecno ndizo simu zilizoshinda katika ushindani huu, Nimekuwa nikitumia simu ya Tecno Phantom 6 kwa muda wa kipindi cha miezi sita, ilinichukua muda kuizoea simu yangu ya iPhone wakati mwingine ilinibidi kubeba simu yangu ya zamani (Tecno) ninapokuwa safarini kwakuwa simu ya iPhone haimudu kufika safari nzima ukiwa free kutumia Data, kucheza miziki na videos kama ilivyo Tecno. Katika ushindani wa kutunza umeme Tecno imeshinda
3: Kutoa huduma na kujali wateja
Katika hili kampuni ya Tecno imefanikiwa kwa kiasi kikubwa Tanzania kwa kuweza kuweka matawi mengi ya kuhudumia wateja wake na kuanzisha huduma ya Calcare ambayo inamuwezesha mtumiaji kupiga simu na kueleza tatizo la simu yake na kuhudumiwa papo hapo.
4: Kujua Mahitaji ya Wateja Wake
Kitu kimoja nilichokipenda kwa hii kampuni ya Tecno ni kufanya utafiti kwa wateja wake hususani kutambua nini cha kuwapa wateja wao. Ni kampuni chache sana hufikiria kupata maoni kutoka kwa wateja, Lakini kwa kampuni ya Tecno ndio kampuni inayojitolea kufanya Tafiti na kukusanya maoni ya wateja wake kuuliza huduma za bidhaa hizo na kutoa kitu bora zaidi.
Hayo ni baadhi ya mambo muhimu niliyoyaona katoka kampuni ya Tecno, Unaweza kutoa maoni yako hapo chini usisite kutuandikia barua pepe [email protected]