Spotify yazindua huduma zake Afrika, yaanza na Afrika Kusini

Mwandishi Alexander Nkwabi

Kampuni kubwa kabisa ya ku stream muziki duniani ya Spotify imezindua huduma zake Afrika jumanne hii ambapo kwa kuanzia imezindua huduma zake jijini Johanessburg nchini Afrika Kusini.

Huduma iliyozinduliwa inampa mtumiaji siku 30 za kujaribu huduma ya kulipia ambapo baada ya hapo mtumiaji atarudishwa kwenye huduma yenye matangazo ndani yake au atatakiwa alipie rand 60 ili aendelee kupata huduma bila matangazo ya biashara.

Kampuni hii kutoka Sweden ilizinduliwa mwaka 2008 na huduma zake zimekuwa zikipatikana kwenye mataifa takribani 60 duniani kote, na kwa sasa ndio kampuni kubwa kabisa ya ku stream muziki ikiwa na watumiaji takribani milioni 200 bila kujumuisha Afrika ambako huduma zake zilikuwa hazijaanza kupatikana rasmi.

Spotify inatarajia upinzani mkubwa kutoka kwa huduma zingine ambazo tayari zinapatikana  Afrika kwa ujumla hasa nchini Afrika kusini zikiwemo Apple Music, Google Play Music, Simfy Africa na Deezer ambazo zinapatikana nchi nyingi za afrika kwa sasa bila kusahau huduma za ku stream zinazotolewa na baadhi ya makampuni ya simu .

Watumiaji wa Afrika kusini hawatahitaji tena kutumia VPN ili kupata huduma za Spotify japo watumiaji wengine wa nchi zilizobaki za Afrika itabidi waendelee kutumia VPN ili kufaidi Spotify.

Sababu kubwa iliyowafanya Spotify kuchelewa kuleta huduma Afrika ni kasi ndogo ya intaneti kwa nchi nyingi za kiafrika na gharama kuwa kubwa kwa bando za intaneti. Kwa utafiti wao wameona Afrika kusini inafaa kuanzia kwa sababu wana intaneti yenye kazi nzuri na huduma za WI-FI zimesambaa maeneo mengi ukilinganisha na nchi zingine barani humo. Huduma za Spotify nchi Afrika kusini zita stream kwa kasi ya 24kbps na inaweza badilika kutokana na kasi ya intaneti itakayopatikana wakati wa kutumia hasa kwenye maeneo yenye mitandao yenye kasi kubwa.

Uzinduzi huu nchini Afrika kusini umekuja wakati Spotify ikijiandaa kuweka hisa zake kwenye soko la hisa la New York, ambapo itaruhusu wawekezaji na wafanyakazi kuuza hisa zao bila kuhitaji kukuza mtaji.

Akizungumza na waandishi wa Reuters, mkurugenzi mtendaji wa Spotify upande wa  mashariki ya kati na Afrika bwana Claudius Boller alisema “Tunaamini Afrika kusini ni nchi nzuri kwa kuanzia” .

Tunaamini Afrika kusini ni nchi nzuri kwa kuanzia

akaongeza “Tumeangalia ukuaji wa teknolojia na hali nchini Afrika kusini tumeona ni soko zuri la muziki na muhimu duniani”

Bwana Claudius Boller amasema pia wana mpango wa kupanua wigo kwa nchi zingine za afrika japo hakuzitaja ni nchi zipi zinazofuata wala ni lini nchi zaidi zitaongezeka.

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive