Telegram yashushwa mara bilioni 1 na zaidi, Whatsapp yahusika

Mwandishi Alexander Nkwabi
Programu tumizi mashuhuri kwa kutuma na kupokea jumbe ya Telegram yashushwa mara bilioni 1 na zaidi. Telegram imekuwa programu ya 15 kuingia kwenye klabu ya app zilizoshushwa zaidi ya mara bilioni moja, ikiwa nyuma ya WhatsApp, Messenger, Facebook, Instagram, Snapchat, Spotify na Netflix.

kwa mujibu wa mtandao wa techcrunch, ripoti hii imetolewa na taasisi inayojihusisha na ufuatiliaji wa mitandao ya kijamii ya Sensor Tower (ambao huwa hawafatilii apps zinakuja zikiwa zimesanikishwa tayari kwenye simu).

Telegram yenye makao makuu yake huko dubai, ilianzishwa mwaka 2013 ikiwa kama mpinzani namba moja wa programu ingine ya WhatsApp, imefikia mafanikio haya siku ya ijumaa . Kwa mujibu wa Sensor Tower, Telegram inachukua 22% ya programu zilizosanikishwa kwenye simu huko nchini India, ambako ndio ina watumiaji wengi zaidi ikifatiwa na Urusi na Indonesia zenye asilimia 10 na 8 kila moja.

Telegram imewezaje kushushwa zaidi ya mara bilioni moja?

Kwanza kabisa telegram ni app moja nzuri sana, inafanya kazi kama inavotakiwa, haimbani sana mtumiaji na ina vitu vingi vingine ambavyo vinakosekana kwenye app zingine zinazofanya kazi sawa na hii.

hata hivyo umaarufu wa telegram umeongezeka kwa kiasi flani ukichangiwa na WhatsApp, ambayo kwa sasa ndiyo programu tumishi maarufu zaidi duniani ya kutuma na kupokea ujumbe. Miezi michache iliyopita, WhatsApp inayomilikiwa na facebook imeshutumiwa kwa kuwa na sera zisizo linda faragha ya watumiaji ikiwemo sera inayowalazimisha watumiaji  ku share taarifa zao na mtandao wa facebook.

Jambo hili limewafanya watumiaji wengi waamue kuachana nayo japo kwa upande wa matumizi ni rahisi kutumia kama inavotakiwa, na kutafuta njia au program zingine mbadala.

Telegram 400m MAUs

Telegram ndio imeibuka kidedea kama app mbadala na hii imesababisha kuongezeka kwa kasi kwa watumiaji wapya hasa kutoka nchi zenye watu wengi wakiongozwa na India ambayo ndio nchi yenye watu wengi zaidi duniani na hii ndio sababu namba moja kuipandisha Telegram mpaka hapo ilipofika.

Japokuwa Telegram imeshushwa mara bilioni 1 haina maana ina watumiaji hai bilioni moja. Telegram ina watumiaji hai takribani milioni 500 kila mwezi, na inawezekana watumiaji hai wameongezeka kwa kipindi hiki ambacho sera za WhatsApp zimekuwa sio rafiki.

Telegram inajitahidi kufanya maboresho kila mara kwa kuleta vionjo mbalimbali kama video calls, kushiriki skrini na vingine vingi, na kuanzia mwezi wa tatu mwaka 2021 walianzisha mfumo kama wa ClubHouse wa voice chat.

Ni app gani unayoipenda kwa ajili ya kutuma na kupokea message? Tuandikie kwenye sehemu ya ku comment hapo chini.

 

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive