Tigo, Selcom na Mastercard waungana kuleta huduma ya Masterpass QR nchini Tanzania

Mwandishi Alexander Nkwabi

Tigo Tanzania kupitia huduma yake ya Tigo Pesa wameungana na kampuni ya malipo kwa njia ya kielektroniki ya Selcom na Mastercard kuleta huduma ya Masterpass Quick Response (QR).

Ushirikiano huu umetangazwa kwenye Kongamano kubwa kabisa duniani la Mobile World Congress (MWC 2018) na kuifanya Tigo kuwa kampuni ya kwanza ya simu kutoa huduma hiyo ambapo wateja wataweza kufanya malipo mahala popote intakapoonekana nembo ya  Mastercard Quick Response

tigo Tanzania ambayo ina takribani watumiaji milioni saba waliosajiliwa na huduma ya tigo Pesa wataweza kufanya manunuzi kwa njia hii salama zaidi kuanzia mwezi nne mwaka 2018 kwa scan code ya Quick Response iliyopo kwa wauzaji kupitia app ya Tigo pesa iliyo kwenye simu janja zao. Hata hivyo watumiaji wa simu za kawaida hawakuachwa nyuma kwani watatumia menyu ya USSD na wataingiza namba ambazo zipo kwa muuzaji.

Simon Karikari, ambaye ni Meneja wa Tigo Tanzania alisema Tigo Pesa sio tu huduma ya kuweka na kutoa fedha, bali ni mfumo unaowezesha wateja kupata huduma mbalimbali za kifedha akaongeza Masterpass ni ongezo jipya kwenye huduma zinazotolewa na TigoPesa ili kuendelea kuwarahisishia maisha yao ya kila siku.

Raisi wa Mastercard tawi la Sub-Saharan Africa bwana Raghav Prasad amesema muungano huu ni hatua moja kubwa katika kuboresha usalama kwa wateja linapokuja swala la miamala. Akafanunua zaidi kuwa Afrika karibu asilimia 85 ya manunuzi ya rejareja yanafanyika kwa cash, mfumo salama na unaopatikana kiurahisi ndio jibu sahihi juu ya tatizo hilo.

“Tunahitaji kuhama kutoka malipo kwa cash kwenda kwenye njia ambazo ni salama, na Tigo Pesa wanakuletea huduma ya Masterpass QR ili kufanya ndoto hii kuwa kweli”

“Tunahitaji kuhama kutoka malipo kwa cash kwenda kwenye njia ambazo ni salama, na Tigo Pesa wanakuletea huduma ya Masterpass QR ili kufanya ndoto hii kuwa kweli”

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
3 Comments
Receive Mtaawasaba notifications Click ‚ÄėReceive,‚Äô then ‚ÄėAllow‚Äô when prompted. Dismiss Receive