Twitter ina mpango wa kuruhusu mtu yeyote kuwa verified

Mwandishi Emmanuel Tadayo

Akizungumza kupitia huduma ya Twitter ya Periscope Livestream, bwana Jack Dorsey ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Twitter amesema kwamba wako mbioni kuruhusu watumiaji wote wa mtandao huo wa kijamii kupata huduma hiyo ya kuthibitishwa.

Hapo awali, Twitter walipotambulisha huduma huu maarufu kama “alama ya bluu” ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya kuonyesha taarifa au maelezo yaliyothibitishwa tu, ambapo alama ya bluu ilitolewa kwa akaunti za watu mashuhuri na wenye ushawishi katika jamii kama vile Wasanii, Viongozi, Wanaharakati, Waandishi, Taasisi & Jumuiya na n.k.

Mwaka 2016 Twitter waliruhusu mtu yeyote kuomba akaunti zao kuthibitishwa, ila Twitter ilihitaji watumiaji hao kutoa sababu za msingi kwa nini wanahitaji akaunti zao kuthibitishwa. Ili mradi wawe waandishi, wabunifu au watu wakubwa wenye ushawishi, ndo maana watumiaji wa kawaida wa Twitter mara nyingi maombi yao ya kuthibishwa hayakufaulu.

Nia yetu ni kufungua uthibitisho kwa kila mtu

”Nia yetu ni kufungua uthibitisho kwa kila mtu,” anasema Dorsey. ”Na kufanya hivyo kwa njia inayoweza kutenga ambapo watu wanaweza kuthibitisha ukweli zaidi kuhusu wao wenyewe na hatupaswi kuwa hakimu au kuwa na ubaguzi wowote kwa upande wetu.”

Dorsey hakufafanua zaidi huo mchakato wa kuthibitisha akaunti za watumiaji utakavyokuwa, ila jumuiya nyingine za mtandao kama vile Airbnb akaunti yako ili iweze kuthibitishwa zinahitaji watumiaji wake kuwasilisha akaunti zao za facebook, namba za simu, anwani ya barua pepe au ID ya picha iliyotolewa na serikali.

WATUMIAJI WANADHANI WANAPOTHIBITISHWA NI KAMA WAMEAMINIWA, KUMBE SIO TUNAVYOAMAANISHA.

Dorsey anaongeza, kwamba kukujulikana na kutojulikana ni sehemu kitu muhimu sana kwa Twitter pia anasisitiza kwamba Twitter haimlazimishi mtu yeyote kuweka taarifa zake halisi kama jina, namba za simu bali tunataka iwe jukwaa ambalo mtumiaji atajisikia huru kulitumia  kuzungumza chochote alichonacho pasipo kuweka taarifa binafsi ambazo kwa namna moja au nyingine zinaweza kumuingiza kwenye matatizo. Pia ameongeza kwamba timu yao inafanya kazi kubwa kuzifuatilia kwa ukaribu akaunti wanazozitilia mashaka kuacha kutoa taarifa za uongo ikibidi kuzuia machapisho yao.

Viongozi wa Twitter kuzungumza live kupitia periscope ni moja kati taraibu walizojiwekea kuzungumza mafanikio na changamoto wanazopitia, mfano kwenye kikao hiki Dorsey alikutana na viongozi wengine wa Twitter kuzungumza masuala ya usalama ya watumiaji, na jinsi gani wanakabiliana na taarifa za uongo kwenye mtandao wao pia maudhui mabaya amabyo yapo kinyume cha sheria. Dorsey aliahidi kuwa makini na taarifa zisizo na ukweli kutochapishwa ingawa hakueleza ni njia gani watatumia.

”Tunakazi nyingi mbele yetu ambayo hatutaweza kuimaliza kwa usiku mmoja. Tutajitahidi kuwa mtandao ulio wazi kadri tuwezavyo.” alisema Dorsey.

Kitu hicho labda kinaweza kisiwe na chema sana kwetu na kinaweza kutuathiri sisi kwa njia nyingi ila tutajitahidi kufanya kila tuwezalo tuwe chombo kilicho wazi kwenu watumiaji na kuelezana  yote tunayokumbana nayo pamoja na changamoto zetu.

 

Mwandishi Emmanuel Tadayo Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
mwandishi wa habari za teknolojia kwenye tovuti pendwa ya mtaawasaba
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive