‎Twitter inafanyia majaribio CoTweets Kukuruhusu kuTweet Pamoja na Marafiki‎

Mwandishi Emmanuel Tadayo
Twitter imeanza kujaribu uwezekano wa kuruhusu watumiaji kuchapisha tweets pamoja. Kipengele hiki kimepewa jina la CoTweets, kipengele hiki kitaruhusu mtu zaidi ya mmoja kushirikiana kuandika tweet. Kwa sasa ni watumiaji wachache wa Twitter waliochaguliwa nchini Marekani, Canada, na Korea ndio pekee wanaweza kutumia kipengele hiki. Hapa kuna yote unayohitaji kujua kuhusu kipengele kipya katika majaribio.

Twitter inafanyia majaribio kipengele cha CoTweets

Kama jina linavyopendekeza, kipengele cha CoTweet  kitaruhusu watumiaji wa Twitter kushirikiana na mtu mmoja au zaidi kwenye tweets. Kupitia kipengele hiki, watumiaji wawili wa Twitter wanaweza kuandika tweet kwa pamoja. Iwapo waandishi wawili watakaoshirikiana kuandika tweet, basi tweet hiyo itaonekana kwenye profile za washiriki wote kwa pamoja.

Kwa kuanzia, mwandishi wa kwanza ataanzisha CoTweet na kisha atamualika mwandishi mwingine. Mwandishi wa pili anaweza kuchagua kukubali au kukataa mwaliko. Cha kusisimua zaidi waandishi wote wanaweza kuiondoa tweet kama wataamua hapo baadae hata kama imeshachapishwa. Ikitokea hali kama hiyo basi ile tweet itabadilika na kuwa tweet ya kawaida kutoka kwa mwandishi wa kwanza aliyeianzisha.

“Tunafanyia majaribio CoTweets kwa muda mfupi kujua ni namna gani watu binafsi na makampuni wanaweza kutumia kipengele hiki ili kuongeza wafuasi na kuboresha mahusiano kwenye akaunti tofauti tofauti. Haya yamesemwa na Msemaji mkuu wa Twitter akiongea na  TechCrunch.

Kipengele hiki sio kipya kwenye mitandao ya kijamii kwani kinafanana na Collab ya Instagram. Mwaka jana Instagram walizindua kipengele cha Collab  kinachokuruhusu kushirikiana machapisho ya post na Reels na watumiaji wengine. Na sasa CoTweet inakuja rasmi basi tutarajie tweet za kusisimua kutoka kwenye akaunti zitazoshirikiana kwa siku za usoni.

Kwa mujibu wa Twitter, majaribio ya co-tweeting yatafanyika kwa muda mfupi, na kampuni imedokeza kuwa inaweza zima kipengele hiki majaribio haya yatakapokamilika na wanaweza kuondoa CoTweets zote zilizotengenezwa kipindi cha majaribio. Tuambie, uko tayari kutumia kipengele hiki kipya kutoka Twitter? Tuandikie mawazo yako kwenye sehemu ya kuandika maoni.

Avatar of emmanuel tadayo
Mwandishi Emmanuel Tadayo Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
mwandishi wa habari za teknolojia kwenye tovuti pendwa ya mtaawasaba
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive