WhatsApp inaweka muonekano mpya kwenye Audio call

Imeandikwa na kasomi
Whatsapp Inaweka Muonekano Mpya Kwenye Audio Call
WhatsApp inaweka muonekano mpya kwenye Audio call, kupitia akaunti ya WaBetaInfo wametangaza kufanya maboresho mbalimbali ya programu hiyo tumishi kwa upande wa toleo la majaribio upande Android na iOS kitu ambacho hivi sasa kimeanza kuonekana kwa watu wachache (beta testers).

Kwa mujibu wa ripoti, watumiaji wa WhatsApp ya Android toleo la beta 2.22.5.4 wanaweza kuona mabadiliko haya kwa upande wa audio call. na watumiaji wachache wa toleo la beta 2.22.5.3 nao wanaweza ona mabadiliko haya.

Mabadiliko haya yalianza kuonekana kwa mara ya kwanza mwezi disemba na ilikuwa ni kwa watumiaji wote wa android na ios. Imeleta muonekano mpya na wa kuvutia zaidi kwa watumiaji.

Whatsapp Android Beta New Voice Calling Interface Screenshot Wabetainfo Whatsapp

 

Acha Ujumbe