Xiaomi kuingia kwenye soko la simu Marekani mwishoni mwa 2018

Mwandishi Alexander Nkwabi

Kampuni ya utengenezaji wa simu ya Xiaomi kutoka China inajiandaa kuingia soko la simu nchini Marekani mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni wa 2019. Xiaomi ambayo ni moja ya makampuni makubwa kabisa duniani ya kutengeneza simu miaka ya hivi karibuni imetanua soko lake mpaka India, kusini mashariki mwa Asia, hispania, ulaya mashariki na sasa wanataka kuingia soko la Marekani.

Ripoti mpya iliyochapishwa na jarida la Wall Street Journal linamnukuu Mwenyekiti wa Xiaomi bwana Lei Jun aliesema kuwa “wana mpango wa kuingia soko la marekani mwishoni mwa 2018 au mwanzoni mwa 2019”

Hata hivyo Xiaomi sio ngeni kwa wamarekani maana tayari wamekuwa wakiuza bidhaa za kielektroniki nchini Marekani kama Android TV  boxes, kamera, spika bila kusahau headphone, lakini hawakuwahi kuingia kwenye soko la simu. Kampuni chache za kutengeneza simu za nje ya marekani zimefanikiwa kuteka soko hilo zikiongozwa na Samsung ya Korea kusini. Kwa upande wa China kampuni ya ZTE imefanikiwa kuwa ya nne kwa uuzaji nchini marekani.

Changamoto kubwa inayowasubiri Xiaomi ambayo pia inawakumba makampuni mengine ya simu kutoka China nchini Marekani ni katazo la serikali ya Marekani kwa wananchi wake kutotumia bidhaa za China kwa sababu za kiusalama wa taarifa zao.

Endelea kuwa nasi @Mtaawasaba na pia usisahau kutufuata katika Social network mbali mbali kwa jina la mtaawasaba, Pia usisahau kusubscribe kwa barua pepe kuweza kupata habari mpya kila zinapoingia, Pia usisite kutoa maoni yako hapo chini! Ahsante sana

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive