App ya YouTube Vanced yafungwa na Google

Mwandishi Emmanuel Tadayo
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, leo ile App maarufu ya YouTube Vanced yafungwa na waendeshaji wake baada ya kutishiwa kufikishwa kortini na Google.

Kama wewe ni mtumiaji mkubwa wa Android, basi utakuwa umewahi kuisikia hii app ya YouTube Vanced.

Kwa kifupi tu YouTube Vanced ni toleo la YouTube lililochakachuliwa ili kukuwezesha kupata huduma zote anazopata mtumiaji wa YouTube Premium lakini bila kulipia chochote. Baadhi ya faida zinazoambatana na app hii ni pamoja na kupata uwezo wa kuangalia video kwenye mtandao wa YouTube bila kukatishwa na matangazo yanayojitokeza kabla na baada ya video kuanza.

Vanced pia iliwapa uwezo kuongeza manjonjo kwenye App ya YouTube ambapo App halisi haikuweza hasa kwenye simu mkononi, manjonjo kama kubadili app kuwa nyeusi kabisa (muonekano wa giza), mengine ni kama kurudisha kitufe chenye idadi ya dislike, kuendelea kusikiliza hata kama umetoka kwenye app (background play), kuondoa sehemu za video zisizo za muhimu kama matangazo ya wafadhili, mengine mengi zaidi. Pia uwezo wa kuruhusu simu za Huawei ambazo zimezuiwa kupata huduma za Google kuzipata tena.

Wakiongea na mtandao wa The Verge kuhusu barua waliyopewa na Google ya kuiondoa app hiyo, wamiliki wa app hii ya Vanced walisema, “tumetakiwa kuondoa neno YouTube”, kubadilisha logo na kuondoa viunga vyote vinavyohusu bidhaa za YouTube.

Wamiliki wa YouTube Vanced waliandika kupitia telegram na twitter kuhusu kuacha kuendeleza huduma za app hii.

Wamiliki wa Vanced pia waliongeza kusema, watumiaji wa Vanced YouTube ambao wameshasanikisha na wanatumia app hii wataendelea kupata huduma mpaka hapo itakapoacha kufanya kazi, ila wao kama wamiliki hawataendelea kutoa matoleo mapya.

Kwa sasa ukifungua tovuti ya YouTube Vanced utakutana na ujumbe usemao, “Vanced is no longer available.” ukimaanisha app hii haipatikani tena.

Mbadala wa YouTube Vanced

Waswahili wanasema kuvunjika kwa mpini sio mwisho wa kulima, kuna app zingine ambazo zinafanya kazi na zinafanana na Vanced kwa kiasi kikubwa. Chini hapo nimezi orodhesha.

 

Mwandishi Emmanuel Tadayo Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
mwandishi wa habari za teknolojia kwenye tovuti pendwa ya mtaawasaba
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive