MtaawasabaMtaawasaba
  • Habari
  • Simu
  • Android
  • Kompyuta
  • Windows
  • Maujanja
  • StartUps
Mengineyo
  • Muongozo
  • Maujanja
  • Programu
  • Simu Janja
  • Teknolojia
Mtaawasaba
  • Kuhusu Sisi
  • Sera ya faragha
  • Vigezo na Masharti
  • Wasiliana Nasi
Mitandao
  • Facebook
  • Twitter
  • Instagram
  • YouTube
  • Newletters
© 2013 - 2023 Mtaawasaba Interactive
Unasoma Serikali ya Tanzania kushusha ada ya leseni za maudhui mtandaoni kwa asilimia 50
MtaawasabaMtaawasaba
  • Apple
  • kompyuta
  • Maujanja
  • Apps
  • StartUps
  • Magari
  • Mtaawasaba
    • Habari
    • Makala
    • Apps
    • Maujanja
    • Kompyuta
    • Simu Janja
    • Magari
    • Matukio
    • Muongozo wa mtumiaji
    • Mitandao ya kijamii
    • Programu
    • Teknolojia
    • Mfumo endeshi
    • Miwani Janja
    • Saa Janja
    • Televisheni
    • Utamaduni
  • Mengineyo
    • Microsoft
    • intaneti
    • Windows
    • SnapChat
    • TTCL
    • Tigo Tanzania
    • vifurushi visivyo rasmi
    • Google
    • halotel
    • Instagram
    • iOS
  • Kuhusu Mtaawasaba
    • Kuhusu Sisi
    • Sera ya faragha
    • Vigezo na Masharti
    • Wasiliana Nasi
Una akaunti? Ingia
Tufuate mtandaoni
© 2022 Mtaawasaba Interactive. Haki zote zimehifadhiwa.
Mtaawasaba > Featured > Serikali ya Tanzania kushusha ada ya leseni za maudhui mtandaoni kwa asilimia 50

Serikali ya Tanzania kushusha ada ya leseni za maudhui mtandaoni kwa asilimia 50

Imeandikwa na Emmanuel Tadayo Miaka 2 iliyopita
Sambaza
Serikali ya Tanzania kushusha ada ya leseni za maudhui mtandaoni kwa asilimia 50
Serikali ya Tanzania kushusha ada ya leseni za maudhui mtandaoni kwa asilimia 50. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania, Innocent Bashungwa amesema Serikali iko mbioni kuondoa 50% ya ada za tozo mbalimbali za leseni kwenye marekebisho ya Kanuni za maudhui ya mtandaoni na maudhui ya utangazaji katika redio na televisheni yaliyofanywa hivi  karibuni ili kuzalisha ajira na vipato  wananchi.

Mabadiliko hayo ya ada yanakusudiwa kufanywa kupitia kanuni za maudhui mtandaoni za mwaka 2020 ambazo ziko chini ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta namba 306.

Katika rasimu ya mabadiliko ya kanuni hizo ya mwaka 2021 ambayo imetolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Serikali inapendekeza kupunguza ada ya sasa ya leseni ya maudhui ya mtandaoni ya kila mwaka kutoka Sh1 milioni ya awali hadi Sh500,000.

Unaweza Kusoma

Elon Musk ametangaza rasmi vita na Apple

Ramani, kutoka Tanzania yakusanya $32m kurahisisha mnyororo wa usambazaji

Teknolojia ya hali ya juu kutumika katika Kombe la Dunia la FIFA Qatar 2022

Tovuti ya iCloud ya Apple yapata muonekano mpya, inavutia zaidi.

Ameongeza kuwa ada kwa Leseni za ‘simulcasting’ imeondolewa kabisa ambapo ameeleza kwamba hatua hiyo imefikiwa baada ya kuzingatia maoni ya wadau ya kuiomba Serikali tahfifu ya ada husika ili waweze kumudu kulipa bila faini au kulimbikiza madeni ambapo amesema watoa huduma wanatazamiwa kuongezeka kutokana na viwango vya ada kuwa rafiki.

Baadhi ya mambo muhimu katika Marekebisho ya Kanuni za Maudhui ya Utangazaji – Redio na Televisheni ni pamoja na kuongeza ukomo wa vituo vya usikivu kwa leseni za wilayani kutoka kimoja hadi vitatu (3) katika eneo ambamo redio au televisheni ipo ambapo ameeleza kuwa marekebisho haya yanatazamiwa kuongeza usikivu wa redio na Televisheni katika maeneo yenye  milima na mabonde.

Aidha, Kanuni ya 37 ya mwaka 2018 imerekebishwa kwa kufuta kanuni ndogo ya (2) iliyozuia kuungana na kituo kingine ili kutoa matangazo (hookup) bila kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ambapo kwa sasa kituo kitatakiwa kinatoa taarifa tu kwa TCRA tofauti na awali.

Kwenye Kanuni ya 37(4) serikali imeondoa masharti ya mgeni kusindikizwa studio kwa lengo la kuondoa kabisa masharti yaliyotaka mgeni wa kituo chochote cha huduma ya maudhui kutoruhusiwa kutembelea kituo hicho mpaka awe ameongozana na Afisa wa Serikali au TCRA

Kwa upande wa  Kanuni za maudhui ya Mtandaoni, mambo muhimu yaliyofanyiwa marekebisho katika Kanuni hizo kuwa ni pamoja na kuondoa masharti kwa watoa huduma wa Internet Cafes (Kanuni ya 2 na 13), kuondoa masharti ya kuwa na leseni kutokaTCRA (Kanuni ya 3), kuondoa Leseni za ‘Simulcasting’ ambapo mtoa huduma wa maudhui ya mtandaoni kwa simulcasting hatalazimika kukata leseni nyingine wala kulipia ada tofauti anaporusha maudhui yaleyale anayorusha katika redio au televisheni asilia.

Pia, kuondoa wajibu kwa watoa huduma kutunga sera ya matumizi na kufunga vifaa vya kuchuja maudhui mabaya (kanuni ya 9), kuondoa zuio la ‘Simulcasting’ kwa redio za wilayani na mikoani na kuondoa zuio la matangazo ya Betting.

Sambaza chapisho hili
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Telegram Barua Pepe Nakili kiungo Durufu
Acha Ujumbe

Toa Jibu Ghairi kujibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Mtaawasaba Newsletter

Jiunge nasi kwa njia ya barua pepe tukujulishe kila inapotoka habari mpya

Zaidi Kutoka Mtaawasaba

Sasa unaweza pata Blue Tick kwa kulipia Instagram na Facebook

Sasa unaweza pata Blue Tick kwa kulipia Instagram na Facebook

Siku 4 zilizopita
Airtel yawa ya kwanza kuzindua huduma ya kadi za eSIM Tanzania

Airtel yawa ya kwanza kuzindua huduma ya kadi za eSIM Tanzania

Siku 5 zilizopita
Instagram yazindua Notes, Candid Stories, na Zaidi

Instagram yazindua Notes, Candid Stories, na Zaidi

Miezi 3 iliyopita
Umoja wa Ulaya waishinikiza Apple kuruhusu maduka mbadala ya programu kwenye iPhones na iPads

Umoja wa Ulaya waishinikiza Apple kuruhusu maduka mbadala ya programu kwenye iPhones na iPads

Miezi 3 iliyopita

© 2013 - 2023 Mtaawasaba Interactive. Crafted by Simba Creative

  • Kuhusu Sisi
  • Sera ya faragha
  • Vigezo na Masharti
  • Wasiliana Nasi
Go to mobile version
logo logo
Karibu Mtaawasaba!

Jaza taarifa kuingia Kwenye Akaunti Yako

Umesahau Nywila?