Elon Musk mbioni kuinunua Twitter kwa Dola bilioni 43

Mwandishi Amos Michael
Ni siku kadhaa tangu atangaze kununua asilimia 9.2 ya hisa za Twitter ambazo ni sawa na dola za kimarekani billioni 2.89 na kumfanya kuwa ndiyo mmiliki mkubwa wa hisa za kampuni hiyo. Taarifa zinasema Elon Musk mbioni kuinunua Twitter kwa Dola bilioni 43, lengo lake kubwa ni kuifanya iwe kampuni binafsi.

Katika tangazo lilichopashwa na US Securities and Exchange Commission imeandikwa, Musk ametoa ofa ya dola 54.20 kwa kila hisa ya Twitter, ambayo ni sawa na asilimia 54 zaidi ya bei ya kawaida ya hisa za kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa jarida la Bloomberg, Musk, mwenye utajiri wa dola za kimarekani bilioni 260, anaweza kumudu kuinunua kampuni ya Twitter ambayo ina thamani ya dola za kimarekani bilioni 37 bila kutetereka.

Siku chache zilizopita, Elon Musk aligoma kujiunga na bodi ya wakurugenzi wa Twitter akiwa kama mdau mwenye nyingi zaidi, haikufahamika ni kwa nini ila sababu kubwa imejulikana ni kuwa kama angekubali basi uwezo wake wa kununua hisa zaidi ungeishia asilimia 14.9 tu hivyo ingemzuia kutimiza lengo lake la kuinunua kampuni nzima.

Musk ambaye ana wafuasi takribani milioni 80 ni mmoja wa watumiaji wakubwa wa Twitter akiungana na Barack Obama, Taylor Swift, Justin Bieber, Katy Perry na Lady Gaga. Aliandika kwa kusikitika kuwa watumiaji maarufu kama “@taylorswift13 hajaandika kitu kwa miezi mitatu” na “@justinbieber ameandika mara moja tu tangu mwaka uanze”.

Mwandishi Amos Michael Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
Meezy ni mchangiaji wa machapisho mbalimbali hapa Mtaawasaba tangu kuanzishwa kwake. Meezy ni mpenzi wa Android na anapokuwa nyumbani hupendelea kupiga kinanda na kuandaa muziki
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive