Google yazindua kituo cha kwanza cha maendeleo ya bidhaa barani Afrika

Mwandishi Alice
Kampuni kubwa ya teknolojia ya Google yazindua kituo cha kwanza cha maendeleo ya bidhaa barani Afrika katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi. Kituo hiki cha maendeleo ya bidhaa kilichozinduliwa leo ni cha kwanza cha kampuni hiyo kuzinduliwa katika bara la Afrika.

Kituo hiki kipya cha maendeleo ya bidhaa kitasaidia kuunda bidhaa na huduma zitakazoleta mabadiliko kwa watu wa Afrika na duniani kote. Tayari, Google imetangaza fursa kwa watu zaidi ya 100 wenye vipaji katika uwanja wa teknolojia katika kipindi cha miaka 2 ijayo ili kusaidia kutatua changamoto ngumu na za kiufundi. Fursa hizi zitawahusu wahandisi wa programu, mameneja wa bidhaa, wabunifu wa UX na watafiti ili kuweka msingi wa ukuaji wa kituo hicho katika miaka ijayo.

Tangazo hili linakuja miezi 7 baada ya kampuni hiyo kuahidi kuwekeza dola za kimarekani bilioni 1 barani Afrika katika kipindi cha miaka mitano ijayo katika hafla yake ya Google for Africa mwezi Oktoba mwaka jana. Katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Sundar Pichai alisema watawekeza katika miradi ambayo itasaidia kuleta ukuaji wa teknolojia barani Afrika.

Tangu wakati huo imefungua kituo cha utafiti cha Google AI huko Accra, Ghana kusaidia kuendesha ubunifu. Mwezi uliopita, pia ilitangaza kuwa Equiano, kebo yake ya mtandao wa subsea, itawasili Togo, kisha Afrika Kusini, Namibia, Nigeria na St Helena zitafuata.

Google inatabiri kuwa Afrika itakuwa na watumiaji wa intaneti milioni 800 na theluthi moja ya idadi ya watu walio chini ya umri wa miaka 35 ifikapo mwaka 2030, na inataka kuwa mstari wa mbele katika harakati hii kwa kufanya kazi na “watu wenye nguvu, ubunifu, na ushirikiano ambao wanaweza kusaidia kutatua changamoto ngumu na muhimu za kiufundi, kama vile kuboresha uzoefu wa smartphone kwa watu barani Afrika”.

Google sasa imejiunga na orodha inayoongezeka ya makampuni makubwa ya teknolojia kama Microsoft na Visa ambayo yamezindua utafiti na maendeleo, na vituo vya uvumbuzi huko Nairobi, Kenya, kwa mtiririko huo.

#ffffff; text-decoration-thickness: initial; text-decoration-style: initial; text-decoration-color: initial;">

Kama unahisi una kipaji, uzoefu, na uko tayari kufanya kazi na Google barani Afrika, unaweza kubofya hapa ili kuona fursa mbalimbali zilizotangazwa na Google.

Mwandishi Alice Mhariri Mkuu
Mitandao ya Kijamii
Alice ni mwandishi na mhariri wa makala mbalimbali hapa Mtaawasaba tangu mwaka 2016. Akiwa hayupo kazini hupendelea kusoma vitabu, kuogelea na kusikiliza muziki
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive