M-Pesa yafikisha wateja milioni 50

Mwandishi Alexander Nkwabi
Kampuni ya Safaricom ambayo kwa pamoja na Vodacom inamiliki huduma ya kifedha ya M-Pesa imetangaza kuwa, huduma ya M-Pesa yafikisha wateja milioni 50 wanaotumia huduma hiyo kila mwezi na kufanya kuwa ndio huduma ya kifedha kubwa kabisa barani Afrika.

Huduma hii ya kifedha ambayo ilianza miaka takribani 14 iliyopita huko nchini Kenya, kwa sasa inapatikana katika nchi zingine ikiwemo Tanzania, Msumbiji, DRC, Lesotho, Ghana, na Misri.

Mafanikio haya haya huduma hii yanakuja miezi 18 tu baada ya Safaricom na Vodacom kuinunua brand hii kutoka kwa Vodafone ya uingereza. Lengo likiwa ni kuharakisha ukuaji wa huduma za kifedha kwa kutumia simu barani Afrika. Kabla ya hapo kulikuwa na watumiaji wapatao milioni 40 kila mwezi wanaofanya miamala karibu bilioni moja kila mwezi.

Mwaka 2007, Safaricom na vodafone walizindua M-Pesa nchini kenya kama njia ya kusaidia wateja kutuma na kupokea pesa papo kwa papo. Kwa haraka sana huduma hii ilipendwa na watu wengi kuichagua kama njia yao ya kwanza ya kufanyia miamala, hii ilisababisha kukua haraka kwa huduma hii.

Kukua huku kwa huduma hii kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na sekta rasmi kukubali huduma hii kama njia ya kupokea na kutuma fedha hivyo kuikuza kwa takribani asilimia 55.

Sasa wateja na wafanyabiashara na makampuni ya kifedha wanaweza kutuma na kupokea malipo mbalimbali ikiwemo kulipia bidhaa, kulipia bili mbalimbali, na huduma zingine, pia kutuma fedha kimataifa, kukopa fedha yote haya ukiwa umekaa na simu yako au kupitia mawakala waliotapakaa kila kona ya nchi.

 

Avatar of alexander nkwabi
Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive