Instagram yafunga App za Boomerang na Hyperlapse

Imeandikwa na Alexander Nkwabi
Instagram Yafunga App Za Boomerang Na Hyperlapse
Kwa mujibu wa Ripoti ya Apptopia iliyochapishwa na mtandao wa TechCrunch inasema Instagram yafunga App za Boomerang na Hyperlapse kwenye Apple App Store na Google Play Store. App hizi zinaondolewa siku kadhaa baada ya Instagram kutangaza itaacha ku support app ya IGTV.

Boomarang ilikuwa ni app maarufu ikiwa imeshushwa takribani mara milioni 300 kwenye app store na Google Play, na siku ambayo imeondolewa ilikuwa imeshushwa mara 26,000. Kwa upande wa Hyperlapse ilikuwa inapatikana Apple App Store pekee na ilikuwa imeshushwa mara milioni 23 pekee.

Katika chapisho la blogu ya Instagram ambalo lilithibitisha kuondolewa app ya IGTV, kulikuwa na ufafanuzi wa kwa nini app hizi zinaondolewa, iliandikwa “ni rahisi kwa watumiaji kupata hivi vipengele vyote app kuu.” Kwa kuwa Instagram kwa sasa inavyo vipengele vilivyo kwenye app hizi inaingia akilini kwa nini wameamua kuziondoa.

Instagram haijasema chochote kuhusu kuondolewa kwa App hizi kwenye blogu yake, isipokuwa watu kadhaa wame tweet kuhusu hili ikiwemo Matt Navarra, ambaye ni mshauri wa maswala ya mitandao ya kijamii.

Japokuwa Instagram yafunga App za Boomerang na Hyperlapse, App ya Layout itaendelea kubaki kwenye App Store. Mpaka sasa haiwezekani kuunganisha picha nyingi kwa pamoja moja kwa moja kupitia Instagram.

Acha Ujumbe