Jinsi ya kupata TIN number mtandaoni (2024)

Mwandishi Alice

TIN number kwa kirefu ni Tax Payer Identification Number au kwa kiswahili namba ya utambulisho ya mlipa kodi. Namba hii huhitajika katika shuguli kadha wa kadha hasa kwenye mambo ya usajili wa biashara, leseni ya udereva n.k. Nambari hii ya utambulisho hutolewa na mamlaka ya mapato Tanzania ili kuweza kuwatambua walipa kodi. kupitia makala hii tutakuelewesha Jinsi ya kupata TIN number bila kufika ofisi za mamlaka ya mapato.

Unahitaji nini kukamilisha usajili wa maombi ya TIN namba?

Ili kukamilisha usajili kupitia mfumo wa mamlaka ya mapato utahitajika kuwa na namba ya kitambulisho cha taifa, ambayo hutolewa na National Identity Authority (NIDA). Unaweza kusoma jinsi ya kupata namba ya NIDA online.

Jinsi ya kujisajili kwenye mfumo wa Online TIN Service

Hatua ya 1

Kwa kutumia simu janja au kompyuta fungua tovuti ya mamlaka ya mapato kisha chagua usajili wa TIN, au nenda moja kwa moja kwenye ukurasa wa usajili wa TIN number.

Jinsi Ya Kupata Tin Number Online

Hatua ya 2

Kwa usahihi ingiza namba za utambulisho wa uraia na namba yako ya simu kisha bofya Next

Hatua ya 3

Ukibofya kitufe cha next, mfumo utatuma nywila (password) kwenye namba uliyoandika, password hiyo utatakiwa kuiingiza kisha bofya next

 

Online TIN Services

Hatua ya 4

Mfumo utakutaka kukamilisha usajili kwa kuingiza taarifa kadhaa ikiwemo barua pepe, kisha bofya Submit

Hatua ya 5

Ukikamilisha hatua 4 za mwanzo, mfumo utakutaka kubadili nywila au password yako. Kubadili ingiza ile password ya mwanzo kisha ingiza mpya, halafu bofya Change Password

namna ya kupata tin number online

Hatua ya 6

Sasa unaweza bofya OK na unaweza ingia kwenye akaunti yako ya usajili wa TIN number

Jinsi Ya Kupata Tin Number Online

  • Ingia kwenye akaunti tuliyotengeneza kwenye hatua za mwanzo hapo juu, au bofya kiunga hiki kwenda moja kwa moja.
  • ukifanikiwa kuingia chagua APPLY FOR PIN kwenye menyu ya akaunti yako kama inavooneshwa hapa chini

TIN ONLINE APPLICATION

  • Chagua aina ya TIN unayotaka kutengeneza (Non-Business TIN au Business TIN ) kisha bofya APPLY
  • itatokea fomu ya usajili ambayo utaijaza kwa usahihi ili kukamilisha usajili
  • ili kuona kama namba yako imetengenezwa unaweza kubofya TIN Status.
Mwandishi Alice Mhariri Mkuu
Mitandao ya Kijamii
Alice ni mwandishi na mhariri wa makala mbalimbali hapa Mtaawasaba tangu mwaka 2016. Akiwa hayupo kazini hupendelea kusoma vitabu, kuogelea na kusikiliza muziki

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive