Vitu vya kuzingatia unapotaka kununua simu ya iPhone iliyotumika (2021)

Mwandishi Alexander Nkwabi
Unahitajika umakini wa hali ya juu unapotaka kununua simu ya iPhone iliyotumika, kwani waswahili wanasema ukizubaa unaachwa feri.

Simu za iPhone zimekuwa maarufu sana miaka ya karibuni, na iPhone 13 ni moja ya simu bora kabisa kuachiliwa mwaka 2021. Bei ya Simu hizi uwa imechangamka iwe unataka kununua mpya au unataka ku upgrade kutoka toleo la nyuma.

Kama lengo lako ni kununua simu nzuri ya iPhone bila kutoboa mfuko, basi njia rahisi uwa ni kununua iliyotumika. Changamoto kubwa inayokuja kwa kununua simu ya iPhone iliyotumika ni ubora wa bidhaa unayonunua vs bei utakayolipia, sio hivyo tu, pia hakuna garantii iyo simu itakuwa nzima kwa muda gani tofauti na simu mpya ambazo mara nyingi bei zake zinakuwa zinafanana na hata una uhakika wapi pa kuanzia ikitokea hitilafu yoyote unapoanza kuitumia simu yako.

Aina ya simu zilizotumika

Kabla hatujaenda mbali zaidi, kwanza kabisa tujue aina ya simu zilizotumika. Kiufupi uwa kuna aina mbili ya simu zilizotumika.
  • Refurbished iPhone

ukisikia iPhone refurbished basi ujue ilirudishwa kwa Apple Store kufanyiwa marekebisho ili iwe katika viwango vinavyokubalika kuuzwa. Refurbished iPhone inaweza kuwa ni mpya ila ilipata hitilafu ndogo (mfano ikachubuka au ikapasuka kioo) au iliyotumika. Simu ambazo ni refurbished uwa zinakuja na waranti.
  • Used iPhone

hii ni iPhone iliyotumika na inauzwa kama ilivyo, sana sana uwa inakuwa wamei reset software. Kama ilikuwa na kioo kimepasuka au touch/face ID ina shida basi inauzwa hivyohivyo. Na mara nyingi wauzaji uwa wanasema kwa wateja changamoto ambazo simu hiyo inazo.

Nshawahi kununua simu kadhaa zilizotumika na hazikuwahi kunisumbua

Unaposikia neno “Simu iliyotumika” kitu cha kwanza kinachokuijia kichwani ni “itakuwa ni simu mbovu” au “imemshinda kuitumia anataka amsukumie mtu”. Inawezekana kuna ukweli ila sio lazima iwe hivyo kila wakati. Nshawahi kununua simu kadhaa zilizotumika na hazikuwahi kunisumbua.

Usipokuwa makini mara nyingi unaweza kuuziwa simu mbovu au yenye hitilafu kubwa ambayo gharama za matengenezo zinaweza kutosha kununua simu ingine. Sikatai nshawahi kukutana na bidhaa za namna hiyo pia. Sema kwa sababu najua najua kuhusu simu nagundua mapema na kupotezea.

Leo nimeamua kuandika miongozo hii angalau isaidie katika mchakato wa manunuzi ya simu zilizotumika, mchakato huu unaweza kufaa kuzingatia hata kwa bidhaa zingine kama tableti na kadhalika. Bila kupoteza muda tuanze kuangalia kipengele kimoja baada ya kingine.

Wapi unaweza nunua iPhone iliyotumika?

kuna njia au mahali tatu za kuweza kupata simu za iPhone zilizotumika, sehemu hizo ni pamoja na;

Maduka yanayouza simu

Kama uko dar es salaam, basi kuna maduka mengi yanayojulikana kwa kuuza simu zilizotumika, kuanzia makumbusho, kinondoni mpaka kariakoo. Tembelea maeneo hayo ili uweze jipatia simu. Kwa mikoani mnaweza tuandikia kwenye comment.

Maduka ya mtandaoni

Hapa ukiingia mitandao ya kijamii ya facebook, instagram au Twitter basi utakutana na maduka au watu wanaouza simu zilizotumika. Pia unaweza tembelea tovuti zinazohusika na kuuza bidhaa mbalimbali kama kupatana, Zoom Tanzania, na Tunzaa n.k.

Mkononi

Hii ni njia ingine ambayo unaweza nunua simu yako, kupitia kwa mtu unayefahamiana na e au lah anayeuza simu yake ya zamani.

 

 

 

 

 

 

Hitimisho

Kama utachukua muda, na umakini katika kununua simu ya iPhone iliyotumika unaweza pata simu nzuri na kwa gharama inayoendana nayo.

Pia, zingatia kwamba unaponunua simu iliyotumika uwa hakuna garantii itafanya kazi kama inavotarajiwa, ilo lisikuogopeshe maana najua waty kibao ambao wamenunua iPhone zilizotumika na hawajapata shida nazo japo wapo ambao wamepigwa na ndio maana tumekupa muongozo huu ili kukusaidia usipigwe na wewe.

Kuna lolote nimeliacha? Basi tuandikie kwenye comment hapo chini.

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive