WWDC 2022: MacBook Air yenye Chip ya Apple M2 Yatangazwa

Mwandishi Alice
Moja ya matangazo makubwa leo siku ya kwanza ya WWDC 2022 ni pamoja na, hatimaye MacBook Air yenye Chip ya Apple M2 Yatangazwa. Uzinduzi huu unakuja muda mchache baada ya uzinduzi wa chipu mpya yenye nguvu ya M2 ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa muda sasa na wapenzi wa teknolojia. Naam hatimaye MacBook Air mpya imetngazwa. Inakuja na maboresho na mabadiliko kadhaa ikiwemo notch, kioo angavu na cha kuvutia zaidi, MagSafe na mengi zaidi. Hapa kuna kila kitu unachohitaji kujua kuhusu MacBook Air mpya:

Hatimaye MacBook Air yenye Chip ya Apple M2 Imetangazwa

Kuanzia na muundo, MacBook Air mpya imetengenezwa kwa kutumia 100% ya alumini iliyorejeshwa. Pia ni kifaa cha kwanza cha Apple kutumia chuma kilichoidhinishwa kilichorejeshwa tena. Laptop hii mpya ni nyepesi na ina uzani wa pauni 2.7 tu (~kgs 1.22). Pia, MacBook Air ina unene wa 11.3mm tu, kumaanisha kuwa ni nyembamba zaidi kuliko unene wa mtangulizi wake M1 MacBook Air.

MacBook Air yenye Chip ya Apple M2 inajumuisha kioo chenye teknolojia ya Liquid Retina chenye ukubwa wa inchi 13.6 na bezeli nyembamba na paneli angavu zaidi. Skrini hapa inaweza kufikia niti 500 na inang’aa kwa 25% kuliko ile iliyotangulia. Pia inaweza kutumia hadi rangi bilioni 1 na kamera ya FaceTime ya 1080p katika notch yenye umbo la ndoo sawa na MacBook Pro.

Kompyuta ndogo hii inaendeshwa na chip ya Apple M2 yenye hadi GPU ya 10-core, hadi 24GB RAM, na hadi 2TB ya hifadhi ya SSD. Chip ya M2 inakuja na injini mpya ya media, inayowezesha mitiririko ya 4K na 8K kwa wakati mmoja, injini ya video ya ProRes, na zaidi. Zaidi ya hayo, MacBook Air yenye Chip ya Apple M2 sasa inaweza kuchaji kwa kutumia MagSafe, ambayo inakuja na kebo ya kuchaji iliyosokotwa.

Apple hawajasema ukubwa au uwezo wa betri kwenye tukio au kwenye chapisho la blogi, lakini ilisema kwamba M2 MacBook Air inaweza kudumu kwa hadi saa 18 za uchezaji wa video. Inakuja na chaja mpya ya 35W Dual USB-C kwenye kisanduku. Zaidi ya hayo, inasaidia Chaji ya Haraka kupitia adapta ya nguvu ya 67W, ikiwa na uwezo wa kufikisha 50% kwa dakika 30 pekee.

MacBook Air yenye Chip ya Apple M2

MacBook Air mpya itapatikana katika aina nne za rangi, ambazo ni Silver, Space Grey, Starlight, na Midnight.

MacBook Pro yenye Chip ya Apple M2 Imetangazwa Vile vile

Pamoja na Air, Apple pia imetangaza MacBook Pro ya inchi 13 na chipu ya M2. Hiyo inamaanisha utapata utendaji kazi wa haraka na maisha bora ya betri (hadi saa 20 za uchezaji wa video, kama inavyodaiwa na Apple). Pia inasaidia hadi 24GB ya kumbukumbu iliyounganishwa na uzuri wote wa chipu mpya ya M2.

Bei na Upatikanaji

MacBook Air yenye Chip ya Apple M2 itauzwa kwa bei ya kuanzia ya dola za marekani 1199 (~Tsh 2,793,670) nchini Marekani, huku M2 MacBook Pro itauzwa kwa dola za marekani 1299 (~Tsh 3,026,670). Tutaweka bei za halisi za MacBook Air yenye Chip ya Apple M2 na MacBook Pro mpya inayotumia M2 pindi itakapoanza kupatikana huku kwetu, kwa hivyo endelea kuwa makini kwa masasisho zaidi.

 

Mwandishi Alice Mhariri Mkuu
Mitandao ya Kijamii
Alice ni mwandishi na mhariri wa makala mbalimbali hapa Mtaawasaba tangu mwaka 2016. Akiwa hayupo kazini hupendelea kusoma vitabu, kuogelea na kusikiliza muziki
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive