Microsoft wazindua Windows 11 yenye muonekano tofauti kidogo na uliozoeleka

Mwandishi Alexander Nkwabi
Leo jumanne tarehe 5, kupitia tovuti yao Microsoft wazindua Windows 11, toleo jipya kabisa la mfumo endeshi maarufu zaidi kwenye kompyuta wa Windows. Toleo hili linakuja kama maboresho ya bure kabisa kwa watumiaji wa mfumo endeshi tangulizi wa Windows 10.

ili uweze kuipata Windows 11, itakubidi usubiri mpaka pale kompyuta yako itakapokupa ujumbe wa ku update kupitia Windows Update. Hii itatokea kwa wale wenye kompyuta ambazo zina vigezo vinavyohitajika kuendesha mfumo huu wa Windows 11 tu, na ujumbe utaanza kuonekana majuma kadhaa yajayo baada ya leo.

Njia nyingine ambayo ni rahisi, ni kudownload na setup ya Windows 11 kupitia tovuti ya Microsoft halafu uiweke kwenye flash drive au DVD, kisha kuinstall mwenyewe kwa wakati wako na kwa utulivu.

Mabadiliko ambayo utakutana nayo mara tu utakapoanza kutumia Windows 11
Start menu iko katikati

kwanza kabisa utakutana na Start menu ikiwa katikati ya taskbar ambapo itakuwa na vitufe vingine, ambapo ukiibonyeza itakuletea orodha ya app unazozitumia mara kwa mara, hata hivyo ili kuepuka dhahama ya kubadilisha kabisa muonekano waliouzoea watumiaji, Windows 11 itakuruhusu kurudisha start button upande wa kushoto ulipozoeleka kupitia kwenye settings.

Mabadiliko kwenye muonekano

kama ni mtumiaji mzoefu wa mfumo endeshi wa Windows, basi utagundua mabadiliko hayo ya muonekano kuanzia kwenye vitufe mpaka mipangilio imekuwa ya kuvutia zaidi kuliko mwanzo.

Maboresho kwa watumiaji wa Touchscreen

Watumiaji wa touch screen wameboreshewa zaidi kwani sasaivi mfumo wa Windows 11 unafanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu kwa watumiaji wanaotumia kompyuta zenye kalamu maalumu (stylus).

Mabadiliko kwenye Windows Store

Windows Store imebadilishwa na kuwa Microsoft Store, moja ya maboresho makubwa ni upatikanaji wa app za android kupitia mfumo huu. Sasa ukienda Microsoft store na ukaandika “android apps” utaletewa Amazon App Store ambayo ukiinstall itakuwezesha kudownload na kuinstall apps za Android.

Hitimisho

sio watumiaji wote wataweza kupata toleo hili hasa watumiaji wa kompyuta za zamani kidogo. Kama kompyuta yako ni ya zamani unaweza kubaki na Windows 10 au unakunua kompyuta mpya.

 

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive