Nokia 1 yenye Android Oreo (Go edition) yazinduliwa kwenye kongamano la MWC

Alexander Nkwabi Add a Comment 549 Views

Utangulizi

Tayari kongamano la MWC 2018 limeanza na makampuni yameanza kutangaza bidhaa wanazozindua, na MHD Global wameanza kwa kutangaza Nokia 1 yenye Android Oreo, ambayo ni simu ya bajeti ndogo inayotumia Android Oreo Go Edition.

Nokia 1 yenye Android Oreo

Simu hii inatarajiwa kuuzwa kwa dola za kimarekani 85 ambazo ni takribani shilingi laki 2 za kitanzania. Itaanza kuuzwa kuanzia mwezi wa nne 2018. Simu hii inakuja na rangi mbili Nyekundu na bluu iliyokoza.

nokia-1

Muonekano wake kwa nje ni wa kawaida kabisa, Simu hii imetengezwa kwa kava la plastiki na kava la nyuma linalotoka linalokuja kwa rangi mbalimbali.

Ukiacha Nokia 1, pia HMD Global wametangaza simu zingine ikiwemo Nokia 7 Plus, Nokia 8110 4G huku wakithibitisha kuwa Nokia 6 toleo la 2018 itaanza kuuzwa ulaya miezi kadhaa ijayo. Simu ambayo inatarajiwa kuwa gumzo ni Nokia 8 Sirocco ambayo nayo imetangazwa leo.

nokia-1-2

Sifa za Nokia 1

  • kioo chenye upana wa inchi 4.5
  • Kamera yenye 5-megapixel na LED flash
  • kamera ya selfie yenye 2-megapixel
  • Mfumo endeshi ni Android Oreo Go
  • Betri inayotoka yenye 2,150 mAh
  • Sehemu mbili za kuweka laini
  • Uwezo wa kucheza musiki na Redio ya FM
  • Prosesa ni Quadcore 1.1GHz
  • Ujazo wa 8GB  (ambao unaweza kuongzwa kwa memori card ya mpaka 128GB)

Endelea kubaki nasi ili tukupashe taarifa mbalimbali kuhusu kongamano la MWC 2018. Pia kwa kutufuata kwenye mitandao ya kijamii, na usisahau ku subscribe ili uwe wa kwanza kupata Habari, Uchambuzi na Makala mbali mbali za kisayansi na teknolojia. Pia usisahau ku acha maoni yako hapo chini na unaweza ku follow channel yetu ya youtube

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive