MtaawasabaMtaawasaba
  • Habari
  • Simu
  • Android
  • Kompyuta
  • Windows
  • Maujanja
  • StartUps
Mengineyo
  • Muongozo
  • Maujanja
  • Programu
  • Simu Janja
  • Teknolojia
Mtaawasaba
  • Kuhusu Sisi
  • Sera ya faragha
  • Vigezo na Masharti
  • Wasiliana Nasi
Mitandao
  • Facebook
  • Twitter
  • Instagram
  • YouTube
  • Newletters
© 2013 - 2023 Mtaawasaba Interactive
Unasoma Simu za Samsung Galaxy A33, A53, na A73 zazinduliwa rasmi
MtaawasabaMtaawasaba
  • Apple
  • kompyuta
  • Maujanja
  • Apps
  • StartUps
  • Magari
  • Mtaawasaba
    • Habari
    • Makala
    • Apps
    • Maujanja
    • Kompyuta
    • Simu Janja
    • Magari
    • Matukio
    • Muongozo wa mtumiaji
    • Mitandao ya kijamii
    • Programu
    • Teknolojia
    • Mfumo endeshi
    • Miwani Janja
    • Saa Janja
    • Televisheni
    • Utamaduni
  • Mengineyo
    • Microsoft
    • intaneti
    • Windows
    • SnapChat
    • TTCL
    • Tigo Tanzania
    • vifurushi visivyo rasmi
    • Google
    • halotel
    • Instagram
    • iOS
  • Kuhusu Mtaawasaba
    • Kuhusu Sisi
    • Sera ya faragha
    • Vigezo na Masharti
    • Wasiliana Nasi
Una akaunti? Ingia
Tufuate mtandaoni
© 2022 Mtaawasaba Interactive. Haki zote zimehifadhiwa.
Mtaawasaba > Featured > Simu za Samsung Galaxy A33, A53, na A73 zazinduliwa rasmi

Simu za Samsung Galaxy A33, A53, na A73 zazinduliwa rasmi

Imeandikwa na Alexander Nkwabi Mwaka 1 uliopita
Sambaza
Samsung Galaxy A33, A53, na A73 zazinduliwa
Yaliyomo
Samsung Galaxy A33 5GSamsung Galaxy A53 5GSamsung Galaxy A73 5GSifa za Samsung Galaxy A33, A53, na A73 (5G)Bei na upatikanaji wa Samsung Galaxy A33, A53, na A73

Ni majuma machache tu tangu kampuni ya simu kutoka korea kusini ya Samsung kuzindua simu za S22, S22 plus na S22 Ultra ambazo ni za hadhi ya juu sana, kwenye tukio la Galaxy Unpacked 2022. Leo wamezindua simu tatu za bei “nafuu” ambazo ni toleo la A, ambapo Simu za Samsung Galaxy A33, A53, na A73 zazinduliwa rasmi. Simu zilizozinduliwa ni toleo la 5G. Kwa mujibu wa taarifa simu ya  Galaxy A53 5G itaingia sokoni Aprili 1, huku zilizobaki zitaanza kupatikana kuanzia Aprili 22. Simu hizi zitapatikana kwa baadhi ya masoko duniani kutegemeana na eneo ulipo.

Simu za Samsung Galaxy A33, A53, na A73 zinakuja na prosesa mpya, kamera zenye akili ya kubuni (AI), betri inayosemekana kudumu mpaka siku mbili, ulinzi ulioboreshwa na mfumo endeshi wa Android ukiwa umevalishwa toleo jipya la ngozi ya OneUI kutoka Samsung.

Unaweza Kusoma

Elon Musk ametangaza rasmi vita na Apple

Ramani, kutoka Tanzania yakusanya $32m kurahisisha mnyororo wa usambazaji

Teknolojia ya hali ya juu kutumika katika Kombe la Dunia la FIFA Qatar 2022

Tovuti ya iCloud ya Apple yapata muonekano mpya, inavutia zaidi.

Samsung Galaxy A33 5G

Samsung Galaxy A33 5G
Samsung Galaxy A33 5G

Simu ya Galaxy A33 5G inakuja ikiwa na ukubwa sawa na A33, inakuja na kioo chenye upana wa inchi 6.4 na refresh rate ya 90 Hz. Kioo chake ni FHD+ na kikiwa na teknolojia ya Super AMOLED. Simu hii imeboreshwa kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na mtangulizi wake A32 pia ina kioo bora zaidi ya simu zingine zilizotoka mwaka huu ambazo ni  Galaxy A23 na M33.

Upande wa kamera, simu hii inakuja na kamera sensa nne, ya msingi ni yenye 48mp na lenzi ya f/1.8. pia ina ultra wide sensa yenye 8mp, kamera ingine ni 5mp macro lenzi, na 2mp depth sensa. kamera ya mbele ni 13mp ambayo iko ndani ya kitobo chini ya kioo.

Sifa zingine zinafanana na A53 5G, ikiwemo betri yenye ukubwa wa 5,000mAh ambayo inajaa ndani ya masaa mawili kwa kutumia chaja yenye 15w.

Samsung Galaxy A53 5G

Samsung Galaxy A53 5G
Samsung Galaxy A53 5G

Galaxy A53 5G inakuja na kioo chenye upana wa inchi 6.5 kikiwa na FHD+ bila kusahau refresh rate ya 120Hz. Kamera ya selfie ni 32mp ikiwa chini ya kioo kilichokatwa kwa mtindo wa duara ujulikanao kama punch hole.

Kamera kuu inakuja na sensa yenye 64MP na lenzi yenye f/1.8. Pia inakuja na kamera ya ultra wide yenye sensa ya 12mp (f/2.2). kamera ingine ni macro yenye 5MP ya mwisho ni 5MP depth sensa. Sifa hizi zinaweza zisiwe maboresho makubwa kwa watumiaji wa A52 ila ni maboresho makubwa kwa simu ya midrange ya mwaka 2022.

Betri ya A53 5G ni 5000mAh ambayo ni ongezeko la 500 mAh kwenye A52. Betri inajazwa na chaja yenye uwezo wa 25W, sawa na Galaxy S22 yenye betri ndogo ya 3,700 mAh.

Samsung Galaxy A73 5G

Samsung Galaxy A73 5G
Samsung Galaxy A73 5G

Samsung Galaxy A73 5G ndio kubwa kuliko zote tatu, ukubwa wake ni inchi 6.7 na kioo chenye teknolojia ya AMOLED kikiwa na FHD+ na 120Hz refresh rate ambayo ni maboresho kutoka kwa mtangulizi wake A72 iliyokuwa na 90Hz.

Simu hii inakuja na kamera kuu yenye sensa yenye 108 megapixel yenye f/1.8. Kamera ya ultra wide ina sensa yenye 12 MP, pia kamera yenye 5 MP depth sensa. kamera yenye 5 MP macro lenzi. kwa mbele kuna kamera ya selfie yenye 32MP chini ya kioo kwenye mkato wa punch hole.

Betri ya Galaxy A73 5G inabaki vilevile 5,000 mAh na uwezo wa kumudu chaja yenye 25W, betri hii ina ukubwa sawa na A33, A53 na hata A23.

Samsung Galaxy A73 5G itapatikana kwa baadhi ya masoko duniani kunazia Aprili 22, sifa zingine, bei na upatikanaji zimeorodheshwa chini.

Sifa za Samsung Galaxy A33, A53, na A73 (5G)

Galaxy A33 5G Galaxy A53 5G Galaxy A73 5G
SIM Single SIM (Nano-SIM) au Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by)
Kioo Super AMOLED, 90Hz, 6.4 inches, 1080 x 2400 pixels, 20:9 ratio (~411 ppi
density), Corning Gorilla Glass 5
Super AMOLED, 120Hz, 6.5 inches, 1080 x 2400 pixels, 20:9 ratio (~405 ppi density),
Corning Gorilla Glass 5
Super AMOLED+, 120Hz, 6.7 inches, 1080 x 2400 pixels, 20:9
ratio (~393 ppi density)
Mfumo endeshi Android 12, One UI 4.1
CPU Octa-core (2.4 GHz & 2.0 GHz) Octa-core (2.4 GHz & 1.8 GHz)
Ukubwa wa hifadhi na RAM
  • 128GB 6GB RAM,
  • 128GB 8GB RAM,
  • 256GB 8GBRAM
  • Expandable: microSDXC
  • 128GB 6GB RAM,
  • 128GB 8GB RAM,
  • 256GB 8GB RAM
  • Expandable: microSDXC (shared SIM)
Kamera
  • Wide: 48 MP
  • Ultrawide: 8 MP
  • Macro: 5 MP
  • Depth: 2 MP
  • Video: [email protected],[email protected]/120fps
  • Selfie: Wide: 13 MP
  • Selfie Video: [email protected]
  • Wide: 64 MP
  • Ultrawide: 12 MP
  • Macro: 5 MP
  • Depth: 5 MP
  • Video: [email protected],
    [email protected]/60fps
  • Selfie: Wide: 32 MP
  • Selfie Video: [email protected],
    [email protected]
  • Wide: 108 MP
  • Ultrawide: 12 MP
  • Macro: 5 MP
  • Depth: 5 MP
  • Video: [email protected],
    [email protected]/60fps
  • Selfie: Wide: 32 MP
  • Selfie Video: [email protected],
    [email protected]
Sensa Fingerprint (side-mounted)
accelerometer, gyro, compass
Virtual proximity sensing
Fingerprint (under
display, optical),
accelerometer, gyro,
proximity, compass
Viunganishi Wi-Fi 802.11 a/b/g/n/ac, dual-band, Wi-Fi Direct,
hotspotA-GPS, GLONASS, GALILEO, BDSUSB Type-C 2.0, USB On-The-Go
Wi-Fi 802.11 a/b/g/n/ac,
dual-band, Wi-Fi Direct,
hotspotA-GPSUSB Type-C 2.0, USB
On-The-Go
Betri Li-Po 5000 mAh, isiyotoka, uwezo wa chaja ni 25W
Rangi Kijivu, Nyeusi, bluu na pichi kijivu, nyeupe na mint

 

Bei na upatikanaji wa Samsung Galaxy A33, A53, na A73

Kwa mujibu wa mtandao wa Price in Tanzania, Galaxy A33 5G inatarajiwa kuuzwa kwa Shilingi 1,100,000 , wakati A53 Galaxy A53 5G inatarajiwa kuuzwa kwa Shilingi 1,300,000 , huku Galaxy A73 5G inatarajiwa kuuzwa kwa Shilingi 1,650,000. Hata hivyo bei hizi sio rasmi ni makadirio tu, endelea kutembelea ukurasa huu kwani tutaongezea bei itakapokuwa rasmi. Kama uko nchi za marekani na ulaya unaweza ku pre order kuanzia leo kupitia Samsung.com, ila kwa Tanzania haijajulikana bado simu hizi zitaanza kupatikana lini.

KWENYE Galaxy A33, Galaxy A53, Galaxy A73, Samsung Galaxy
Sambaza chapisho hili
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Telegram Barua Pepe Nakili kiungo Durufu
Acha Ujumbe

Toa Jibu Ghairi kujibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Mtaawasaba Newsletter

Jiunge nasi kwa njia ya barua pepe tukujulishe kila inapotoka habari mpya

Zaidi Kutoka Mtaawasaba

Sasa unaweza pata Blue Tick kwa kulipia Instagram na Facebook

Sasa unaweza pata Blue Tick kwa kulipia Instagram na Facebook

Siku 4 zilizopita
Airtel yawa ya kwanza kuzindua huduma ya kadi za eSIM Tanzania

Airtel yawa ya kwanza kuzindua huduma ya kadi za eSIM Tanzania

Siku 5 zilizopita
Instagram yazindua Notes, Candid Stories, na Zaidi

Instagram yazindua Notes, Candid Stories, na Zaidi

Miezi 3 iliyopita
Umoja wa Ulaya waishinikiza Apple kuruhusu maduka mbadala ya programu kwenye iPhones na iPads

Umoja wa Ulaya waishinikiza Apple kuruhusu maduka mbadala ya programu kwenye iPhones na iPads

Miezi 3 iliyopita

© 2013 - 2023 Mtaawasaba Interactive. Crafted by Simba Creative

  • Kuhusu Sisi
  • Sera ya faragha
  • Vigezo na Masharti
  • Wasiliana Nasi
Go to mobile version
logo logo
Karibu Mtaawasaba!

Jaza taarifa kuingia Kwenye Akaunti Yako

Umesahau Nywila?