Snapchat kuruhusu watumiaji kubadili username

Mwandishi kasomi
Mtandao wa kijamii pendwa kwa vijana wa Snapchat kuruhusu watumiaji kubadili username kuanzia Februari 23 mwaka huu. Kampuni hiyo imetangaza leo kuwa watumiaji wake watakuwa na uhuru wa kubadili username kama ilivyo katika mitandao mingine ya kijamii kama Instagram na Twitter.

Mabadiliko haya hayataweza kuathiri maeneo mengine ya akaunti ya mtumiaji kama orodha ya marafiki, Snap codes, Snap scores, memories, na mengineyo. Mtandao wa The Verge umeripoti kuwa Kuanzia juma lijalo watumiaji wote wa android na iOS duniani kote wataweza kubadili username zao.

Kipengele hiki kimekuwepo kwa watumiaji wa Snapchat nchini Australia kwa muda sasa. Na sisi wengine tuliobakia tutaruhusiwa kuanzia juma lijalo. Na ili uweze kubadili username yako, fungua Snapchat kisha nenda kwenye Settings > Username > Change Username.

Badili jina snapchat 2

Hata hivyo Snapchat wameandika kuwa hutaweza kubadili username zaidi ya mara moja kwa mwaka. Pia Snapchat imesema hautaweza kubadili username ambayo uliwahi kuitumia au ambayo kuna mtu anaitumia. Username ambayo umeibadilisha hautaweza kuirudia tena hata kama hakuna mtu anayeitumia.

 

 

Avatar of kasomi
Mwandishi kasomi Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
Mwandishi | mhamasishaji | mwanafalsafa | blogger | Host | Personalty TV & Radio presenter @Kasomi TV
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive