MtaawasabaMtaawasaba
  • Habari
  • Simu
  • Android
  • Kompyuta
  • Windows
  • Maujanja
  • StartUps
Mengineyo
  • Muongozo
  • Maujanja
  • Programu
  • Simu Janja
  • Teknolojia
Mtaawasaba
  • Kuhusu Sisi
  • Sera ya faragha
  • Vigezo na Masharti
  • Wasiliana Nasi
Mitandao
  • Facebook
  • Twitter
  • Instagram
  • YouTube
  • Newletters
© 2013 - 2023 Mtaawasaba Interactive
Unasoma TECNO wazindua Spark 8 yenye chip ya Helio P22
MtaawasabaMtaawasaba
  • Apple
  • kompyuta
  • Maujanja
  • Apps
  • StartUps
  • Magari
  • Mtaawasaba
    • Habari
    • Makala
    • Apps
    • Maujanja
    • Kompyuta
    • Simu Janja
    • Magari
    • Matukio
    • Muongozo wa mtumiaji
    • Mitandao ya kijamii
    • Programu
    • Teknolojia
    • Mfumo endeshi
    • Miwani Janja
    • Saa Janja
    • Televisheni
    • Utamaduni
  • Mengineyo
    • Microsoft
    • intaneti
    • Windows
    • SnapChat
    • TTCL
    • Tigo Tanzania
    • vifurushi visivyo rasmi
    • Google
    • halotel
    • Instagram
    • iOS
  • Kuhusu Mtaawasaba
    • Kuhusu Sisi
    • Sera ya faragha
    • Vigezo na Masharti
    • Wasiliana Nasi
Una akaunti? Ingia
Tufuate mtandaoni
© 2022 Mtaawasaba Interactive. Haki zote zimehifadhiwa.
Mtaawasaba > Featured > TECNO wazindua Spark 8 yenye chip ya Helio P22

TECNO wazindua Spark 8 yenye chip ya Helio P22

Imeandikwa na Alexander Nkwabi Miaka 2 iliyopita
Sambaza
tecno spark 8
Yaliyomo
Utangulizi: Spark 8Muonekano wa Spark 8Kamera za Spark 8Ndani ya Spark 8Upatikanaji na Bei ya TECNO Spark 8Hitimisho

Utangulizi: Spark 8

Kampuni ya simu ya Tecno leo imezindua simu ya gharama nafuu ya Spark 8 ambayo ni muendelezo wa toleo lililopita la Spark 7 ambayo ilitoka mapema mwanzoni mwa mwaka 2021. Simu ndio simu ya kwanza kuachiliwa ikiwa na nembo ya “Stop at Nothing” iliyoanza kutumika hivi karibuni.

Simu hii inaungana na simu zingine kutoka familia ya TECNO ikiwemo Phantom X, Camon 17 Pro na Spark 7P ambazo tayari ziko sokoni.

Unaweza Kusoma

Elon Musk ametangaza rasmi vita na Apple

Ramani, kutoka Tanzania yakusanya $32m kurahisisha mnyororo wa usambazaji

Teknolojia ya hali ya juu kutumika katika Kombe la Dunia la FIFA Qatar 2022

Tovuti ya iCloud ya Apple yapata muonekano mpya, inavutia zaidi.

Kampuni hii ya China inazidi kuteka soko la simu kwa nchi za kiafrika hasa kwa kujikita kwenye kuachia simu za gharama nafuu. Kampuni hii yenye mtindo wa kuachia simu hizi bila kuzitangaza, hivyo basi usishangae kukutana na simu hii madukani bila kuwa na matangazo yoyote.

Muonekano wa Spark 8

kimuonekano, simu ya Spark 8 inakuja na kioo cha IPS LCD chenye upana wa inchi 6.5 na uwezo wa kuonesha picha za HD+ zenye mpaka ukubwa wa 1600 X 720. Juu ya kioo kuna kamera ya selfie yenye umbo la chozi (tear drop) na upande wa nyuma ina kamera kubwa mbili na flashi, pia kuna sensa ya fingerprint.

tecno spark 8

 

Kamera za Spark 8

inakuja na kamera kubwa yenye uwezo wa kupiga picha zenye ukubwa wa 16 MP na kamera ndogo yenye kupiga picha zenye ubora hafifu za QVGA.

Upande wa mbele, kuna kamera kwa ajili ya picha na video yenye uwezo wa kupiga picha zenye ukubwa wa mpaka megapizel 8

Tecno Spark 8

Ndani ya Spark 8

Spark 8 inakuja na RAM yenye ukubwa wa GB 2, huku ikiwa na nafasi ya hifadhi yenye ukubwa wa hadi GB 64 ambapo inaweza kuongezwa kwa kutumia microSD. pia ina Helio P22 chipset ambayo ni maboresho ya mtangulizi wake Spark 7 iliyokuwa na Helio A25 chipset.

Simu hii inaendeshwa na mfumo endeshi wa android 11 Go edition ukiwa ndani ya HiOS 7.6. Unaosukumwa betri yenye ukubwa wa 5000mAh yenye kuchajiwa na chaja ya watts 10 kupitia port ya usb. ina uwezo wa kupokea simcrad mbili, 4G LTE, WI-FI, GPS bila kusahau ina sehemu ya kuchomeka earphone (3.5mm audio jack)

Helio P22 Chipset

Upatikanaji na Bei ya TECNO Spark 8

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali, simu hii tayari imeanza kuuzwa nchini Nigeria na kuanzia juma hili itaanza kupatika katika nchi zaidi za Afrika ikiwemo Tanzania.

Upande wa bei, tarajia kuipata simu hii kwa shilingi za kitanzania 340,000.

Hitimisho

Simu ya Tecno Spark 8 ni simu ya gharama nafuu iliyolengwa kwa watumiaji wenye matumizi madogo mpaka ya kawaida.

Endelea kuwa nasi kwa kutufuata kwenye mitandao ya kijamii na chaneli yetu ya youtube

 

KWENYE Android Go, Spark 8
Sambaza chapisho hili
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Telegram Barua Pepe Nakili kiungo Durufu
Acha Ujumbe

Toa Jibu Ghairi kujibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Mtaawasaba Newsletter

Jiunge nasi kwa njia ya barua pepe tukujulishe kila inapotoka habari mpya

Zaidi Kutoka Mtaawasaba

Sasa unaweza pata Blue Tick kwa kulipia Instagram na Facebook

Sasa unaweza pata Blue Tick kwa kulipia Instagram na Facebook

Siku 4 zilizopita
Airtel yawa ya kwanza kuzindua huduma ya kadi za eSIM Tanzania

Airtel yawa ya kwanza kuzindua huduma ya kadi za eSIM Tanzania

Siku 5 zilizopita
Instagram yazindua Notes, Candid Stories, na Zaidi

Instagram yazindua Notes, Candid Stories, na Zaidi

Miezi 3 iliyopita
Umoja wa Ulaya waishinikiza Apple kuruhusu maduka mbadala ya programu kwenye iPhones na iPads

Umoja wa Ulaya waishinikiza Apple kuruhusu maduka mbadala ya programu kwenye iPhones na iPads

Miezi 3 iliyopita

© 2013 - 2023 Mtaawasaba Interactive. Crafted by Simba Creative

  • Kuhusu Sisi
  • Sera ya faragha
  • Vigezo na Masharti
  • Wasiliana Nasi
Go to mobile version
logo logo
Karibu Mtaawasaba!

Jaza taarifa kuingia Kwenye Akaunti Yako

Umesahau Nywila?