Telegram Premium inakuja ikiwa na stika na reaction za kipekee

Mwandishi Alexander Nkwabi
Telegram ni moja ya programu maarufu zaidi za kutuma ujumbe. Programu hii inasifika kwa usalama na faragha ya message zinazotumwa. Programu hii ambayo ni ya bure, sasa inaonekana inahitaji kujiingizia kipato ili kuweza kujiendesha. Miezi michache ilopita walianzisha kipengele cha matangazo ya biashara kwenye channel mbalimbali. Na sasa kampuni hii inaachia bidhaa mpya ya Telegram Premium. Telegram Premium inakuja ikiwa na stika na reaction za kipekee kwa watumiaji wake tu ambapo watumiaji wa kawaida hawataweza zipata.

Japokuwa Telegram hawajatoa maelezo kuhusu program hii mpya, bei au upatikanaji wake, ila siku za karibuni walizindua toleo la 8.7.2 beta kwenye simu za iPhone na kuanzisha kipengele cha kujisajili kiitwacho Telegram Premium. Usajili utawawezesha watumiaji kupata na reactions mbalimbali za kulipia.

telegram premium 1 telegram premium 2 telegram premium 3 telegram premium 4 telegram premium 5

Kwa sasa toleo la Telegram Premium linapatikana kwenye mfumo endeshi wa iOS pekee lakini kwa mujibu wa taarifa siku si nyingi watumiaji wa android pia wataanza kupata. Kwa mujibu wa Android Police, waligundua kuwa watumiaji wa toleo la bure hawakuweza kupata stika badala yake walipata ujumbe wa kuwataka kujisajili kwenye Telegram Premium kupata stika na reaction zaidi.

Telegram hivi karibuni iliachia sasisho kubwa, na kuanzisha vipengele kadhaa vipya kama vile sauti za arifa maalum, muda maalum wa kunyamazisha, menyu ya kufuta kiotomatiki katika maelezo mafupi, na zaidi.

Nini maoni yako kuhusu Telegram Premium? Je, uko tayari kulipa ada ya kila mwezi kupata kama stika za kipekee na reactions? Hebu tujue katika maoni hapa chini.

 

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive