Umoja wa nchi za Ulaya kulazimisha matumizi ya USB-C kwa simu zote, na vifaa vingine

Mwandishi Alexander Nkwabi
Kamisheni ya Ulaya, ambayo ndio msimamizi wa sheria wa umoja wa nchi za ulaya, umepitisha mswada ambao kama utapishwa utakuwa sheria itakayolazimisha matumizi ya chaja za USB-C kwa simu zote, makampuni yanayotengeneza simu na vifaa vingine vya kielektroniki yatatakiwa kutengeneza simu zenye port zenye kuingiza chaja za USB-C

Lengo la mswada huu ni kuondoa uchafuzi, na kufanya maisha ya watumiaji wa vifaa vya kielektroniki kuwa rahisi kwa kuruhusu chaja moja kutumika na vifaa tofauti zaidi ya kimoja.

Sheria hii itatumika kwenye vifaa vingine kama spika zinazobebeka, tableti, headphone, kamera na makampuni yatatakiwa kutumia viwango vya chaja vitakavyokubalika na vifaa vyote. Hata ivyo sheria hii haigusi chaja ambazo ni wireless. Hii ni kwa sababu umoja wa ulaya wanaamini bado kuna ugunduzi mwingi kwenye eneo hilo.

Makampuni mengi ya vifaa vya kielektroniki hasa ya simu za android tayari wanatumia mfumo huu USB-C isipokuwa kampuni ya Apple kwenye simu za iPhone.

Apple hawajafurahishwa na sheria hii

Apple ambao wanatumia USB-C kwenye bidhaa zao kama MacBook na iPad, lakini kwenye simu za iPhone wanatumia chaja maarufu kama lightining chaja.Apple wamekuwa wakilalamikiwa sana kwa kuwanyima watumiaji wa iPhone fursa ya kutumia chaja zingine.

Lakini haya yanaweza kubadilika kufuatia mswada huu mpya. Apple wanaweza kulazimika kubadili na kuanza kutumia chaja za USB-C pia.

Msemaji wa Apple ameandika kuwa wao kama kampuni wanasimamia ubunifu na nini wateja wanataka. Na wanasimama na umoja wa ulaya katika kulinda mazingira. Akaongeza kusema, wanasikitishwa na uamuzi huu wa umoja wa ulaya kwani unazuia ubunifu, na pia utamiza watumiaji wa iPhone kwa nchi za ulaya maana tayari wana simu zenye chaja za lightining, na itakuwa uchafuzi wa mazingira kama watalazimika kuwa na zingine za Type-C.

Nchi za Afrika zitaathirika?

Ulaya inachukua sehemu kubwa ya mauzo kwenye soko la simu janja, kulazimisha kutumia viwango vinavyofanana kwa simu zote kwenye bara hilo hakutaacha salama sehemu zingine za dunia ikiwemo Afrika.

Ili kuondoa usumbufu kuna uwezekano mkubwa wa makampuni kuamua kutumia viwango vya kufanana dunia nzima.

Soko la simu janja hasa zile kwa ajili ya kawaida (midrange) na zile za hali ya juu kwa nchi za kiafrika linakuwa kwa kasi, ambazo ndizo zinazotumia USB-C, hivyo inawezekana kabisa mabadiliko kutokea kwa simu zote.

hitimisho

mswada huu ni sehemu ya mapitio ya mswada wa Radio Equipment Directive ambao utahitaji kupigiwa kura na bunge la ulaya ili kuwa sheria.

kama itapitshwa kuwa sheria, basi makampuni yanayotengeneza simu yatapewa miaka miwili kabla sheria hii haijaanza kuwabana.

Mwaka 2020 bunge la ulaya lilipiga kura kuwe na sheria mpya itakayotaka kuwa na chaja za kufanana kwenye simu na bidhaa zingine za kielektroniki.

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive