Xbox one mpinzani wa playstation 4

Mwandishi Hemedans Nassor

kama wewe ni mpenzi wa video games utakua unajua tayari sony wamezindua playstation 4 na microsoft nao wamezindua xbox one. xbox one sio game tu limezinduliwa na mambo mengi kama tv box, kinetic sensor mpya na games mpya za EA sport.hebu tuliangalie hili game jipya la microsoft lina nini cha muhimu?

Â

HARDWARE

Tofauti na sony ambaye ameeka specification za playstation four kama siri wao Microsoft wameanika wazi specification za xbox one. Game hili litakua na chip za amd nanometer 40 zenye 8 core cpu, ram ni 8gb na hard drive yake ni 500gb. Ina usb port 3.0 na wifi yake ni 802.11. game console hili lina uwezo wa kuplay cd za bluray.

Â

Â

Xbox one sio game tu bali ni top-box lina vitu kama hdmi na tv-box

watanzania tunapenda sana kitu kimoja kinachofanya mambo mengi (multipurpose). Na hili game nalo linafanya mambo mengi tofauti na kuwa game console tu. Ukiwa na xbox one utapata hdmi port (waya wa kupitishia multimedia kutoka kwenye game hadi kwenye tv) ambayo itakuwezesha kuunganisha vitu vyako kama ving’amuzi, receiver za satellite dish, dvd, home theatre vyote hivi. Hii inamaana xbox inaweza kuwa kama kipitishio cha vifaa vyako kwenda kwenye tv.

Haiishi hapo ukiwa na xbox utaweza kuliambia game kitu unachotaka kufanya kwa kutumia sauti. Mfano unaweza liambia open FIFA 2014 game then hapo hapo litafungua hilo game.

Â

Â

SOFTWARE

Xbox inakuja na muonekano kama wa windows 8 na inavitu vingi ambavyo sio vya gamers. Xbox inakuja na apps kama internet explorer na skype .

Muonekano wa xbox ni kama ule wa windows 8

Hili game linasuport multitasking, uwezo wa kurun application zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Ukiwa na xbox unaweza kugawanya kioo na ukafanya mambo mawili. Mfano upo nyumbani munatumia tv moja unaweza gawanya nusu tv ikawa upande unaonesha game na upande unaonesha tv.

GAMES

Xbox imezinduliwa na magame mengi sana yakiwemo FIFA 2014, NBA live 2014, EA sport UFC, call of duty; ghosts na mengineyo. Wamesema jumla kutakua na magame kama 15 yatakayotoka na xbox one.

ARE YOU READY? Messi, Ronaldo, ibracadabra, hazard, vanpersie, falcao

Kuna tetesi kua game zitachezwa online tu na wengine wanasema zitakua online na offline kwa bahati mbaya Microsoft mpaka sasa hajasema habari ipi ni ya kweli.

GAME PAD

Pad ya xbox one itakua ndogo kidogo kuliko ya xbox ya kawaida na pia itakua na rangi nyeusi completely.

Pad ya xbox one ikiwa na muonekano mpya

Pad hii itakua na vibration nne ambazo zitakua zinavibrate tofauti tofauti kutokana na matukio. Mfano kama ni game la gari kuna vibration ya speed kubwa, vibration ya kugonga mwenzako, vibration ya kuwasha gari nakadhalika.

SENSOR MPYA YA KINETIC

Kinetic ni feature ya Microsoft inayofanya mambo mengi kwenye hili game. Hii sensor ndio ambayo inakusikiliza wewe muda wote. Ukisema open tv hii inaskiliza na kuopen tv. Na inafanya kazi hadi maeneo yenye kelele nyingi.

Kinetic mpya inayoreceive voice na camera ya mbele

Hii kinetic sensor pia ina camera ya mbele kwa ajili ya skype na camera hio inasuport full hd 1080p na kizuri zaidi sababu game inakua mbali ina maana ukiongea skype huonekani wewe tu bali na mazingira ya karibu na wewe kama makochi, zulia, meza na madirisha.

Â

Bei ya hii console ni dola 400 around laki 7 kwa Tanzania.

Â

Â

Mwandishi Hemedans Nassor Mchangiaji
Hemedans aka Chief Mkwawa, amekuwa mwandishi wa makala mbalimbali za teknolojia kuanzia kuanzishwa kwa Mtaawasaba. Kwa sasa ni mchangiaji kila anapopata nafasi
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive