Microsoft kuinunua kampuni ya michezo ya video ya Activision Blizzard kwa dola bilioni $68.7

Alice Maoni 27
Ni ghafla tu leo imetangazwa kuwa Microsoft kuinunua kampuni ya michezo ya video ya Activision Blizzard kwa dola bilioni $68.7. Hii ni moja ya hatua ya kuisukuma Microsoft kwenye upande wa michezo ya video, ambapo kama dili hili litakamilika basi Microsoft itakuwa kampuni ya tatu kwa ukubwa kwenye michezo ya video ikiwa nyuma ya Sony na Tencent.

Michezo ya video maarufu iliyochapishwa na Activision Blizzard ni pamoja na “Call of Duty,” “Candy Crush,” “Warcraft,” “Diablo,” “Overwatch” pamoja na “Hearthstone.” Kwa mujibu wa Microsoft, dili hili litasukuma ukuaji wa biashara yao ya michezo ya video hasa kupitia simu za mkononi, kompyuta na itakuwa kama msingi wa maandalizi wa wao kuingia kwenye metaverse.

Dili hii ikikamilika, michezo mipya na michezo ya awali kutoka Activision Blizzard kama WarcraftDiabloOverwatchCall of Duty, na Candy Crush itaanza kupatikana kupitia Xbox Game Pass na PC Game Pass. Mkurugenzi mtendaji upande wa michezo bwana Phil Spencer alifafanua.

Kwa mujibu wa jarida la Wall Street Journal, Mkurugenzi mtendaji wa Blizzard Activision bwaba Bobby Kotick  anatarajiwa kuachia ngazi pindi dili litakapokamilika, ambapo linatarajiwa kuwa mwaka 2023. Hii inakuja baada ya kuibuka kwa maandamano ya wafanyakazi wa Activision Blizzard na baadhi kuacha kazi kwa sababu za kunyanyaswa kingono na zingine kama hizo.

Microsoft wanatarajiwa kukamilisha dili hili kubwa kabisa na Activision Blizzard mnamo mwishoni mwa mwaka wa fedha 2023, hii ina maana itachukua takribani miezi 18 kabla haijakamilika. Muda mrefu utatumika kukamilisha dili hili kwa sababu Activision Blizzard ni kampuni kubwa inayofanya kazi katika masoko mbalimbali duniani ambayo ruhusa mbalimbali za kisheria.

Mwandishi Alice Mhariri Mkuu
Mitandao ya Kijamii
Alice ni mwandishi na mhariri wa makala mbalimbali hapa Mtaawasaba tangu mwaka 2016. Akiwa hayupo kazini hupendelea kusoma vitabu, kuogelea na kusikiliza muziki
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive