Sasa inawezekana kuongeza hadi watu 512 kwenye grupu la WhatsApp

Mwandishi Alexander Nkwabi
WhatsApp imefanya maboresho makubwa kwenye sasisho lake la hivi karibuni ambapo watu wote sasa wataweza kujibu jumbe kwa reactions na maboresho mengi zaidi. Sio hivyo tu kwani Sasa inawezekana kuongeza hadi watu 512 kwenye grupu la WhatsApp. Imetangazwa na WhatsApp inayomilikiwa na Meta kuwa kuanzia sasa ukomo wa wanachama wa vikundi vya WhatsApp utakuwa watu 512.

Ukomo wa Kikundi cha WhatsApp Waongezeka

Chapisho la hivi karibuni la blogu ya WhatsApp linaonyesha kuwa hivi karibuni itaruhusu watumiaji kuongeza hadi wanachama 512 kwenye kikundi. Hii itakuwa ni mara mbili zaidi ya kikomo cha sasa cha wanachama 256 kwa kikundi kimoja cha WhatsApp. Kwasasa kipengele hiki kinapatikana kwa baadhi ya watumiaji, na tunatarajia kufikia watumiaji wote wa Android na iOS hivi karibuni.

Maboresho haya ni jambo la kuvutia hasa kwenye vikundi vinavyojumuisha vikundi vikubwa vya watu. Hata hii ni kiasi cha chini sana cha ukomo ukilinganisha na mpinzani wake ambaye ni Telegram ambayo ukomo wake ni watu 20,000 kwa kikundi.

Pamoja na hayo, WhatsApp pia imeongeza ukomo wa kutuma na kupokea mafaili yenye ukubwa wa mpaka 2GB. Hii ni ongezeko kubwa zaidi kutoka ukomo wa awali ambao ulikuwa ni 100MB pekee. WhatsApp inasisitiza matumizi ya wi-fi unapotuma au kupokea mafaili makubwa. Kipengele hiki kimeanza kwa kupatikana kwenye toleo la beta kwanza.

Kama unavyojua tayari, athari za ujumbe (reactions) pia zimeanza kufikia watumiaji na matoleo ya hivi karibuni ya programu sasa yanawaunga mkono. Watumiaji wanaweza kubonyeza ujumbe kwa muda mrefu na kuchagua kutoka kwa chaguzi 6 za emoji ili kuijibu. WhatsApp imethibitisha kuwa hivi karibuni itaongeza chaguo zaidi za emoji kwenye orodha, kama vile inapatikana kwenye Instagram.

Pia WhatsApp kwa muda sasa wamekuwa wakifanyia kazi vipengele vya Reactions na Community, na sasa wametangaza rasmi kuzindua vipengele hivyo. Haya ndiyo unayotakiwa kuyafahamu. Kupitia  press release waliyoandika, kipengele cha Communities kitakuwa ni mahususi kwa taasisi lama shule na klabu ndogo ndogo, bila kusahau taasisi zinazojitolea.

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive