Jinsi Ya Kuzuia Automatic Updates kwenye Windows 11

Mwandishi Alexander Nkwabi

Ni miezi kadhaa tangu Windows 11 iachiwe.  Microsoft huachia masasisho ambayo hujiweka yenyewe kwenye kifaa chako cha Windows 11 moja kwa moja iwe unapenda au hupendi na hivyo kumaliza data yako huku ukiwa hujui imeishaje.

Ni jambo zuri kwa Kifaa chako kupata Sasisho mpya za usalama lakini kwa upande mwingine imekuwa kikwazo kwa baadhi ya watumiaji wa Mfumo huo wa uendeshaji hasa katika utumiaji wa Data.

 Chapisho litaangazia Jinsi Ya Kuzuia Automatic Updates kwenye Windows 11. Njia hii ni rahisi kabisa Ya Kuzuia Automatic Updates kwenye Windows 11.

Ni jambo zuri kwa Kifaa chako kupata Sasisho mpya za usalama lakini kwa upande mwingine imekuwa kikwazo kwa baadhi ya watumiaji wa Mfumo huo wa uendeshaji hasa katika utumiaji wa Data.

Ikiwa unatumia Windows 11 kwenye kompyuta yako basi  inawezekana kurejesha udhibiti na kuzuia Mfumo wa uendeshaji kupakua na kusakinisha sasisho moja kwa moja kwa kutumia script hii ndogo na rahisi.

Pia unaweza jaribu [irp posts=”23174″ name=”Njia rahisi ya kuzuia Automatic Updates za Windows 10″]

Kupitia njia hii utaweza kuzuia masasisho ya moja kwa moja na kama utataka kurejesha masasisho utaweza pia.

Kwa kuanza unahitaji

  • kompyuta
  • faili lenye skripti ukalolipata hapo chini

Ipakue file hili  kwenye kompyuta yako

cmd file icon

ukishapakua faili hilo, fungua kwa kubofya  Auto-Update-Enable_Disable-Win11 na kisha itaomba ruhusa ya Administration ya kompyuta yako, utakubali kisha ubonyeze Y kwenye keyboard yako

  1. Bonyeza key yoyote kuondoka na mpaka hapo utakuwa tayari umefanikiwa kuzima sasisho za kujiinstall zenyewe kwenye mfumo wako wa uendeshaji.
  2. utakuwa umekamilisha, rahisi eeeeh?
  3. kama utataka kurudisha automatic updates fuata maelekezo hayo hayo hapo juu.

Tufuatilie kwenye mitandao mbali mbali ili usipitwe na Habari, Uchambuzi na Makala mbali mbali ya mitanadoni na ya kiteknolojia kwenye FacebookTwitterInstagram, na Youtube, Pia usisite kutoa maoni yako hapo chini au tuandikie barua pepe kwa barua pepe

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
1 Comment

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive